Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 30 Rabi' II 1442 | Na: 1442/38 |
M. Jumapili, 20 Disemba 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ndugu mheshimiwa / Muhammad Abdullah Yaqoub – mwandishi wa safu ya "Safari ya Mashairi" (Safar Al-Qawafi) katika gazeti la Al-Ahram Al-Yawm
(Imetafsiriwa)
Assalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh,
Kujibu kile kilichoelezwa kwenye safu yako yenye kusomeka "Safari ya Mashairi" (Safar Al-Qawafi) katika gazeti la Al-Ahram Al-Yawm, toleo (2945), la Jumapili tarehe 05 Jumada Al-Awwal 1442 H, sawia na 12/2020 M, chini ya kichwa: "Hizb ut-Tahrir hairidhiki na kuondolewa kwetu kwenye orodha ya ugaidi!!" Tunasema, na Mwenyezi Mungu ndiye Mpeanaji Tawfiq:
Kwanza: Ninakushukuru kwa kuwa na hamu kwako na kile ambacho Hizb ut-Tahrir inachapisha, kama ambavyo tunakushukuru kwa kuchapisha kwako taarifa ya Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Sudan iliyo na kichwa: " Serikali ya mpito yaziba kufeli kwake na furaha kizushi, kwa uamuzi usiofaa wa Amerika ambayo inalipia gharama kubwa kwa kuupiga vita Uislamu na kusawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi," ambayo uliijumuisha kikamilifu katika safu yako pasi na kugeuzwa.
Pili: Maneno yako: (Na tunamwambia Ustadh Abu Khalil, msemaji wa chama kinachotafuta kitu kisichowezekana, kwamba Sudan nzima ina njaa na inaumwa, na ili karibia kufa kwa sababu ya vikwazo hivi vya kidhulma, kwa hivyo je, huwapendelei watu hawa waliodhulumiwa kupata maisha bora, na unajua kuwa njaa ni kafiri ewe ustadh wetu anayeheshimika?) Mimi nasema: Usemi huu unagongana na ukweli na uhalisia, hatutafuti kitu kisichowezekana, kwani hakika Khilafah ilikuwa ni uhalisia uliojaza kheri na uadilifu ulimwenguni kwa zaidi ya karne kumi na tatu, na kwamba kurudi kwake tena baada ya utawala wa kiimla ambao tunaishi ndani yake sasa, na ambao chini ya kivuli chake watu wanakumbwa na njaa na maradhi, umezungumziwa na Mkweli wa wakweli (saw) pindi aliposema:
«... ثُمّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا. ثُمّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»
“…Kisha utakuwepo utawala wa kiimla, na utakuwepo kwa muda apendao Mwenyezi Mungu uwepo, kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume" kisha akanyamaza. Imepokewa na Imam Ahmad katika Musnad yake. Ama kuhusu ukweli kwamba sisi hatuwapendelei watu hawa walioshindwa nguvu kupata maisha bora, jua kwamba haimkiniki kwa Waislamu hawa kuwa na maisha bora isipokuwa chini ya kivuli cha hukmu za Uislamu zenye kutabikishwa na dola ya Khilafah kwa njia ya Utume. Je! Mola Azza wa Jalla hakusema:
[فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى]
“…basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.” [Ta-Ha: 123]?
Je, Mwenyezi Mungu (swt) hakusema:
[وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ]
“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi.” [Al-A’raf: 96]?
Lile lililoifukarisha nchi na waja, na kufanya magonjwa yawasibu, ni kuifuata Magharibi mkoloni kafiri, na kuomba suluhisho kutoka kwake, licha ya utajiri wa Sudan kwa rasilimali zake za dhahiri na zilizofichika, lakini imeporwa na kafiri Magharibi kwa sababu ya ubaraka wa watawala Ruwaibidha, na kujiweka mbali kwao na hukmu tukufu za Uislamu.
Tatu: Maneno yako (Je! Hizb ut-Tahrir inataka nini, ambayo haijasema lolote la kheri tangu alfajiri ya mapinduzi haya yenye baraka), Mwenyezi Mungu (swt) amewaamuru waumini kwa kusema:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلاً سَدِيداً]
“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa.” [Al-Ahzab: 70]. Na Mtume (saw) akawaamuru kwa kusema:
«مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ، وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَلْيَقُلْ خَيْراً أَوْ لِيَصْمُتْ»
“Yeyote anayemuamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze”.
Ama kauli ya kweli ambayo ndio kheri, ni kauli juu ya msingi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah ya Mtume Wake (saw), na sio kauli juu ya msingi wa matamanio, au juu ya msingi wa hadhara ya kikafiri ya Kimagharibi. Na kwa kipimo hiki, hakika Hizb ut Tahrir ndiyo yenye kusema kheri, na wasiokuwa yeye miongoni mwa watu wa matamanio na wapambe, na walinganizi wa hadhara ya kikafiri ya Kimagharibi, wanazungumza kauli batili na ya urongo. Hakika umeidhulumu Hizb kwa makala yako haya, na ikiwa Hizb ut-Tahrir haisema kheri, basi ni nani anayeisema, ewe ndugu yangu?! Kwani hakika kheri, kheri yote iko katika kufuata njia ya Mwenyezi Mungu (swt), na kutabikisha hukmu zake chini ya kivuli cha Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo Hizb ut-Tahrir inailingania, au unataka sisi tuibariki batili, au tuipake mafuta kama wengi wa waliopotea wanavyofanya?
Hakika Hizb ut-Tahrir inalingania kheri na inasema kheri, na inawaamuru watu kwa hilo, kwani hakuna wokovu kwa Umma wala hakuna kheri kwake isipokuwa kwa yale aliyokuja nayo Mtume wetu mtukufu (saw), na kujifunga na yale aliyoyaleta, kama alivyosema Mwenyezi Mungu (swt):
[فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّى يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنْفُسِهِمْ حَرَجاً مِمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيماً]
“La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenykee kabisa.” [An-Nisa’: 65].
Ibrahim Uthman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |