Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 28 Rajab 1444 | Na: HTS 1444 / 34 |
M. Jumapili, 19 Februari 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Wakutana na Mkurugenzi wa Idhaa ya Taifa (Omdurman)
(Imetafsiriwa)
Ndani ya wigo wa kampeni ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan ya kupambana na mihadarati, ujumbe kutoka hizb leo, Jumapili 19/02/2023, kwa uongozi wa Ustadh Ibrahim Othman Abu Khalil - msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, akifuatana na Ustadh Ahmed Abkar, wakili – mwanachama wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, na Maustadh wawili Abd al-Khaliq Abdun na Ibrahim Musharraf, wanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayani Sudan, walikutana na Ustadh Osama Sharif - Mkurugenzi wa Idhaa ya Taifa (Omdurman), kwa uwepo wa maustadh, Salah Al-Tom - Mkurugenzi wa Zamani wa Idhaa hiyo, na Yassin Ibrahim - Mkurugenzi wa Idara ya Vipindi katika Mamlaka ya Kitaifa ya Redio na Televisheni, na Muhammad al-Mahdi Hamed - Idara ya Uhandisi ya Redio ya Kitaifa.
Baada ya kukaribishwa, kiongozi wa ujumbe huo, Abu Khalil, aliutambulisha ujumbe huo, kisha akazungumza kuhusu kampeni iliyoanzishwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan katika Shirika la Habari la Sudan (SUNA) kupambana na mihadarati mnamo tarehe 22/01/2023, na kwamba ziara hii inakuja ndani ya kampeni hii, ikionyesha kuwa mada ya mihadarati sio Wafanyibiashara Waadilifu, wasafirishaji wa mihadarati na watumiaji wa mihadarati, bali ni vita vya vita vya kisasa, vinavyoingia kwenye kile kinachoitwa vita vya kizazi cha tano kwa nia ya kuharibu jamii kwa kuharibu akili za vijana.
Ingawa dola inayohusika katika vita hivi inaweza kufichwa kwa watu, lakini umbile la Kiyahudi lilikuwa wazi kuwa lilihusika katika kuijaza Sudan na mihadarati, na licha ya hayo, serikali inapokea wajumbe wake kwa mikono miwili, badala yake inajaribu kuhalalisha uhusiano nalo, na hii ina maana kwamba haiko makini katika kupigana na mihadarati, na kwamba sio ya kuaminiwa katika vita hivi, kwa hivyo ni muhimu kufanya kazi ya kusimamisha dola ya kimfumo, ambayo ni dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ahadi ya Mola wetu Mlezi (swt), na bishara njema ya Mtume wetu (saw).
Kisha mazungumzo mapana yakafanyika, ambayo kila mtu alishiriki, akithamini dori ya hizb katika kazi hii kubwa, na itifaki ikafikiwa na ndugu, mkurugenzi wa idhaa, katika kuendelea kuwasiliana.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
https://hizbut-tahrir.info/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/sudan/3095.html#sigProId5b04db7f5b
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |