Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ubwana ni Kwa Sheria ya Mwenyezi Mungu (Swt)

Kuna ombwe kubwa la kimfumo kote duniani, ambalo linadhihirika kwa Wamagharibi, kwa kiasi kikubwa kama ilivyo ndani ya ulimwengu wa Kiislamu, ikiwemo Pakistan. Sheria ya mwanadamu, inayodhihirishwa katika zama zetu kuwa ni ya kisekula,  demokrasia huria, inashambuliwa kutokana na kiwango kikubwa cha kutofaulu kwake.  Sheria ya mwanaadamu imepelekea urundikwaji mkubwa  wa utajiri kwenye mikono ya tabaka teule la watawala, kupitia ufanyaji kazi wa ubepari wenyewe na ufisadi.  Matajiri wakubwa zaidi wa dunia wameshuhudia utajiri wao ukipanda kwa asilimia 27.5 kufikia $10.2 trilioni  (£7.9 trilioni) kuanzia Aprili hadi Julai mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti kutoka benki ya Uswisi (UBS).  Kinyume chake, umaskini uliokithiri umekuwa ukiongezeka kwa mara ya kwanza ndani ya zaidi ya miongo miwili, Benki ya dunia imeripoti tarehe 7 Oktoba 2020. Hivi sasa kuna miito ya mageuzi kwa ajili ya usambazaji mpya wa mali, kupitia uhisani na kodi kubwa kwa matajiri, ikiambatana na miito ya mapinduzi,  ukiwemo wito wa Khilafah ambao kwa sasa unatokeza kwa nguvu zaidi kuliko hapo awali kwenye Ulimwengu wa Kiislamu.

Pia ni wazi kuwa Demokrasia si “ya watu, kwa ajili ya watu” kama ambavyo watetezi wake wanavyodai. Uundaji wa sheria ni wa tabaka tawala, kwa ajili ya maslahi ya tabaka tawala. Tabaka tawala lina ubwana juu ya uundaji wa sheria kwa kukidhi maslahi yao, kupitia uunganishaji baina ya utajiri mkubwa na uundaji wa sheria.  Ni watu wa tabaka tawala pekee ambao wana mtaji wa kutosha kufadhili kampeni za uchaguzi za gharama kubwa zaidi, kuzindua wagombea wake waliowachagua kuingia katika bunge la sheria, kama inavyojionesha kwa mfano wa wazi wa kampeni za sasa za uraisi wa Marekani.  Ili kulipa fadhila, wabunge waliochaguliwa wanahakikisha upitishwaji wa sheria kupendelea wafadhili wao wa kifedha na wafadhili wengine, kuhakikisha ubwana kwa ajili ya tabaka teule lenye nguvu.  Ukilinganisha na migogoro ya ndani juu ya ubwana kwa raia au ubwana kwa majeshi ndani ya Pakistan ni kupigania nguvu tu kati ya pande zinazoshindana, ambapo hubadilishana kuhifadhi ubwana kwa maslahi yao.

Kiini cha kufeli kwa demokrasia huria ya kisekula ni kuwa sheria zinaundwa na watu. Kilicho halali au haramu kinaamuliwa na akili ya mwanaadamu, kulingana na fikra ya mwanaadamu yenye kikomo inayoyumbishwa na matakwa na tamaa za kibinadamu. Sheria za mwanadamu zimefungua milango ya udanganyifu kutoka kwa tabaka tawala kwa ajili ya manufaa wanayopata. Tabaka teule la watawala hutengeneza sheria kulingana na kujipendelea wao wenyewe, ikijumuisha na uelewa wao na hekima zilizo na kikomo.  Sheria ya mwanaadamu ndio sababu ya msemo wa mbunge John Dalberg-Acton, “Utawala hupelekea ufisadi, na utawala usio na mipaka hufisidi moja kwa moja.”

Tofauti na ulimwengu wa kimagharibi, Demokrasia si ya lazima kwa Waislamu. Vitisho, uzoefu wa awali wa marekebisho ya Sheria za Kanisa, umewafanya wamagharibi waasi moja kwa moja dhana yoyote inayohusu sheria ya Mungu. Hata hivyo, uzoefu wa ulimwengu  wa Kiislamu kwa sheria ya Mwenyezi Mungu (swt), kupitia mfumo wa utawala wa Kiislamu, Khilafah, ni tofauti kabisa. Wakati katika demokrasia, “utawala ni wa sheria za wanaadamu, kwa ajili ya tabaka tawala,” katika Khilafah, “utawala ni wa sheria za Mwenyezi Mungu (swt), kwa ajili ya watu.” Ya halali na ya haramu yanaamuliwa na Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) pekee, hivyo hufungwa milango ya udanganyifu kwa wale walio madarakani.

Hivyo, chini ya Sheria ya Mwenyezi Mungu (swt), walio madarakani hawatoweza kupindisha sheria kwa manufaa binafsi, kwa vile wamefungwa kutekeleza sheria inayochukuliwa kutoka kwenye Qur’an na Sunnah. Chini ya sheria ya Mwenyezi Mungu (swt), wale walio madarakani wako chini ya sheria ya Mwenyezi Mungu (swt), bila ya kinga itakayowazuia wao kushtakiwa. Chini ya sheria ya Mwenyezi Mungu (swt), Al-Hakiim (Mwenye Busara), Al-‘Aliim (Mwenye ujuzi wa kila kitu), uchumi wa Kiislamu unahakikisha utawanyaji wa mali kwa mujibu wa hukumu zake hasa. Kwa karne nyingi, Khilafah ilitoa kiwango cha hali ya juu cha maisha kwa raia wake wote, bila ya kujali dini zao, ikiwemo huduma bure za afya na elimu.

Bila shaka Ummah wa Kiislamu umebarikiwa kwa sheria ya Mwenyezi Mungu (swt). Ombwe la ulimwengu la sasa ni muwafaka sio tu kwa kurejesha Khilafah kwa njia ya Utume, ni muwafaka kwa Khilafah kujionyesha yenyewe kama mfano kwa wanaadamu wote, ambao wamechoshwa na kuelemewa kwao kutokana na Sheria za Mwanaadamu.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

(أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ)

“Asijue aliye umba, naye ndie Mjua siri, Mwenye habari?” (Al-Mulk 67:14)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb Ut Tahrir na

Musab Umair – Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 19 Novemba 2020 22:33

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu