Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ushuhuda Kumhusu Naveed Butt

#MtambueNaveedButt

#AachiweHuruNaveedButt

Naveed Butt ni sura halisi ya uongozi katika dola ya Khilafah ijayo. Ni miongoni mwa makada wa kisiasa Waislamu wanaokabili kwa ushujaa kila dhoruba ili kuendesha mambo ya watu kwa vizuri. Naveed anabeba dhamira isioyumba na fikra isio ya mapatano linapokuja suala nyeti la kusimamisha Khilafah kuwa ni jukwaa msingi kwa kuhuika kwa Waislamu na suluhisho kwa wanaadamu.

Hawa ni watu wanaohudumia misingi hasa na ni injini kwa harakati zenye umuhimu wa kihistoria.

Naveed amekuwa muda wote na bado hadi sasa ni chimbuko la mvuto kwa wengi na hasa kwangu. Kutekwa nyara kwa Naveed tokea Mei 2012 ni hatua nyengine inayoumiza lakini iliyo muhimu kuelekea njia tukufu ya kusimamisha Khilafah iliobarikiwa.

Mwenyezi Mungu (swt) mlipe mema mengi Naveed Butt kwa kila sekunde anayotumia katika kifungo hichi na mhuishe kwenye utukufu kama alivyohuika Sayyidna Yusuf (as). Amiin.

   [مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu waliotimiza waliyoahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.”   [Al-Ahzab: 23]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Tariq

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 19 Novemba 2020 22:29

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu