Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mafunzo kutoka kwa Maeneo Spesheli ya Kiuchumi ya China

Katika hotuba kubwa huko Shenzhen mnamo 14 Oktoba 2020, Waziri Mkuu wa China Xi Xinping aliadhimisha kumbukumbu ya miaka 40 ya eneo la kwanza kabisa spesheli la kiuchumi la China (SEZ) ambalo lilikuwa ni kipengee kikuu cha mkakati wa wazi na wa mageuzi wa China. "Tunapitia mabadiliko ambayo hayajapatapo kutokea kwa karne moja," Xi alisema katika mji wa Kusini wa Shenzhen, ambao mnamo 1980 uliasisiwa kama eneo spesheli la kwanza la kiuchumi la China.

Wakati Deng Xiaoping alipokuwa kiongozi mkuu wa China mnamo 1978, alirithi uchumi ambao ulikuwa na matatizo mengi. Nchi hiyo ilikwama katika miaka ya 1950, ilikosa maendeleo ya kiteknolojia na ilitegemea viwanda vyenye kuhitaji kiwango kikubwa cha mtaji. Uzalishaji wa bidhaa za matumizi ulikuwa wa chini na bidhaa za kimsingi kama baiskeli, nguo na feni za umeme zilifanyiwa mgao. China ilikuwa nchi masikini, yenye mtaji mdogo lakini nguvu kazi kubwa. Sekta zote zilikuwa mikononi mwa serikali na Kampuni za Serikali (SOEs) hazikuwa na motisha ya kuboresha ufanisi. Jaribio la hapo awali la kukuza China chini ya ukomunisti lilikuwa janga na kwa kufariki Mao Zedong mnamo 1976, chama cha Kikomunisti kiligundua kinahitaji kubadilisha njia.

Mnamo 1980, Beijing iliunda Eneo la kwanza Spesheli la Kiuchumi (SEZ) katika mkoa wa pwani wa Guangdong na Fujian, lililoundwa ili kuvutia uwekezaji wa kigeni katika utengenezaji wa kiwango cha chini kupitia kutoa ardhi ya bei rahisi, nguvu kazi na aina kadhaa za kodi na motisha zingine. Mafanikio katika miji ya kusini yaliruhusu Beijing kupanua mageuzi ya kiuchumi, kwanza hadi eneo la Mto Yangtze na baadaye hadi miji kando ya Bahari za Manjano na Bohai. Kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita, nguzo hizi za pwani zilikuwa kama mpaka wa majaribio wa Beijing (na kufuatiliwa kwa uangalifu) na ulimwengu wa nje. Maeneo ya pwani hatimaye yangetoa utajiri unaohitajika ili kufanikisha maendeleo ya maeneo mapana na duni ya ndani ya China. Kwa kufanya hivyo, walihakikisha utulivu wa kijamii na kwa kuongezea, mshiko wa Chama cha Kikomunisti wa mamlaka.

Maeneo haya spesheli ya kiuchumi (SEZ) yalifanikiwa sana hivi kwamba mnamo 1993, 2000 mengine zaidi yalianzishwa. Haya SEZ yaliruhusu uwekezaji wa kigeni na teknolojia nchini na ikawa chanzo kipya cha utajiri kwa China. Ilisababisha China kuwa uchumi unaolenga kuuza bidhaa nje na kuwa karakana ya kiulimwengu. Mageuzi ya biashara na uwekezaji na motisha ya China yalisababisha kuongezeka kwa Uwekezaji wa moja kwa moja wa Kigeni (FDI) kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1990. Leo Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) umesaidia sana shughuli za kiuchumi na kubuni nafasi za kazi, pia iliruhusu maarifa ya kigeni ya kiufundi na usimamizi kuingia China. Hii ndio sababu hadi leo kampuni zote za kigeni nchini China zinalazimika kuhamisha maarifa ya kiufundi. Tume ya Kutathmini Uchumi na Usalama wa Amerika na China ya 2010, ambayo inalishauri Bunge la Congress la Amerika juu ya maswala ya sera yanayohusiana na China, ilithibitisha hili, kuhusu mikakati ya China ya kukuza wigo wa viwanda vya ndege kwa kusema: 'Mikakati ya Beijing ni pamoja na msaada mkubwa wa serikali kisiasa na kifedha kwa viwanda vya utengenezaji ndege vya China na kuhitaji kampuni za ndege za kigeni kutoa teknolojia na njia za kujua namna ya kupiku kwa badali ya kupata mwanya wa soko.'

China imeweza kukuza uchumi wake kwa kufungua sehemu za nchi kwa kampuni za kigeni, ambazo zinaweza kutumia nguvu kazi ya bei rahisi ya China kuzalisha bidhaa kwa bei rahisi kuliko sehemu yoyote nyengine duniani. Leo IPhone, vipakatalishi vya ulimwengu, pamoja na vifaa vingi vya elektroniki vya watumiaji vyote vinatengezwa China.

Huku mtindo huu wa kiuchumi ukiwa umeleta mafanikio pia umeleta matatizo mengi. China inategemea mataifa ya kigeni kuagiza bidhaa zake za bei rahisi na wakati kunapokuwa mgogoro wa kiuchumi Magharibi kama ilivyokuwa hali mnamo 2008, hii huathiri China. Imeifanywa China kutegemea nishati na bidhaa za ulimwengu kutengeza bidhaa hizi. China imechafua njia zake za maji na hewa ili viwanda vyake kuendelea. China inategemea zaidi uchumi wa ulimwengu kisha Amerika, ambayo inategemea sana matumizi ya nyumbani. Hii ndio sababu China imeathiriwa sana na vita vya biashara na Amerika kwani imefinyangwa mno ndani ya uchumi wa ulimwengu.

Kufeli kukubwa kwa China hata hivyo ni kwamba haina badali kwa uchumi wa ulimwengu wakati wengi wanapoteza imani kwake. Ukosefu wa usawa ulimwenguni, kupotea kwa imani katika demokrasia nk, China haina chochote cha kutoa kwani nchi yake na uchumi haukujengwa kamwe juu ya mfumo wowote. China imeukumbatia uchumi wa ulimwengu, sio kwa sababu za kimfumo, bali kwa sababu ilihitaji kukua vyenginevyo idadi yake ya watu bilioni moja ingeasi chama cha Kikomunisti. Hii ndio sababu China inakabiliwa na shida zile zile za kiuchumi zilizoko magharibi na haiwezi kutoa chochote kipya kuibadilisha.

Mao aligundua baada ya Vita vya Pili vya Dunia kuwa bila ya kuwa huru na kuyatoa mataifa ya kigeni yaliyokuwa yameikalia China wakati wa karne yake ya udhalilishaji kamwe haitaweza kufanikiwa. Lakini kile Mao na wanafunzi wake walishindwa kutambua ni kwamba wameikumbatia thaqafa ya kimagharibi na licha ya ukweli kwamba sasa wanaidhibiti China ikiwa wataukumbatia mfumo badali hawatafaulu tu pekee bali kihakika watakuwa na kitu cha kuupa ulimwengu mbali na mipango ya kibiashara.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Adnan Khan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 18 Oktoba 2020 21:30

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu