Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Watawala wa Pakistan Wanaleta Masimulizi Dhaifu ya Kukwepa Vita Kama Chaguo la Kuikomboa Kashmir

Maadhimisho ya mwaka wa kwanza ya India kubatilisha Kifungu cha 370 na 35A na kuongeza ukandamizaji wa Waislamu wa Kashmir yamepita kwa maneno matupu ya kawaida ya uongozi wa kiraia na kijeshi. Kuipa jina upya barabara kuu ya Kashmir kuwa ni barabara ya Srinagar na nyimbo ya Youm-e-Istehsal (Siku ya Mzingiro) ni mifano ya madoido haya.

Jambo lenye kukera zaidi ni muendelezo wa masimulizi yanayotoka Makao Makuu ya Jeshi kutetea juu ya kutochukua hatua kwao dhidi ya kitendo cha India, mbele ya mbinyo mkali kutoka kwa Ummah wa kutaka utekelezwaji uwe wa kivitendo. Katika mwaka mmoja uliopita, masimulizi haya yaliendelea ikiwa ni muitikio wa kukataliwa kwake na Ummah.

Mwanzo ulikuwa kwa simulizi kwamba vita vyovyote vitapelekea kuenea hadi kuwa vita vya nyuklia ambavyo vitapelekea uharibifu wa kihakika kwa pande zote mbili, na kwa hivyo kusifanyike vita kabisa. Mtu hushangaa kuhusu nini kimefundishwa katika Mafunzo ya Kivita katika Chuo Kikuu cha Kijeshi cha Taifa (NDU) wakati viongozi wa Jeshi la Pakistan waliohitimu kutoka taasisi hii wanapitisha maoni haya. Thaqafa ya kijeshi inayofundishwa katika NDU inaendana na falsafa ya kijeshi ya Kimagharibi ambayo maoni yake ni kukazia kuwa uwepo wa silaha za nyuklia unahakikisha kuwa vita vinaepukwa kutokana na desturi za hali ya kawaida. Historia ya kijeshi iliofuatia 1945 ni ushahidi kwa hili, lakini hatuna haja kwenda mbali ya mvutano wa karibuni baina ya India na China juu ya Bonde la Galwan. Zote India na China, zimekuwa na nguvu za Nyuklia, zimeingia kwenye vita vya muda ambavyo havikupelekea vita vya nyuklia.

Migongano katika msimamo wa uongozi huu umefichuka wakati katika hali ya kujifanya majasiri wanasema kuwa Jeshi la Pakistan litatoa jibu stahili endapo jeshi la India litavuka kuja Azad Kashmir. Hivi jibu stahili halimaanishi kuelekea vita, na kuwa vita katika hali kama hii pia havipelekei kwenye vita vya nyuklia, au kuna baadhi ya sababu maalum zinazojulikana na uongozi wa juu tu kuwa hazitopelekea kutokea hayo?

Ummah uliokataa masimulizi haya ulishibishwa na hadithi za uchumi. Kwa kuzingatia kuwa, tukio la India katika Kashmir la Agosti 5, 2019 limesadifu ujio wa timu ya IMF na FATF nchini Pakistan Agosti 6. Kusadifu huku kumegonga hisia, lakini hadithi ya mgongano kuhusu uchumi ni yenye kugonga zaidi hisia. Serikali iliyofuata baada ya Musharraf imeendelea kuwa katika mipango ya IMF na sambamba nayo Jeshi la Pakistan limekuwa likiendelea kuwa katika vita kwenye maeneo ya makabila. Hivyo kwa nini vita visihimiliwe dhidi ya Wahindi wakati uongozi wa Jeshi la Pakistan umehimili vita vya aibu na kikatili dhidi ya ndugu zetu wenyewe katika maeneo ya kikabila?

Katika kuvunja maelezo haya, udanganyifu sasa umeendelezwa kwa kusemwa kuwa uchumi wa India ni mkubwa zaidi ya uchumi wa Pakistan na unaweza hasa kubeba gharama za vita. Ikiwa ina visa vya virusi vya korona zaidi ya milioni 4, uchumi unaodhaniwa kushuka kwa asilimia 24 katika robo ya kwanza ya 2020-2021 [1], harakati za kujitenga zikiunganishwa na makabiliano ya kijeshi na China, mtu anaweza kuhoji kinyume chake kuwa uchumi wa India uko katika hali mbaya na kwa kweli unaweza kuvurugika kutokana na vita vya Kashmir. Hata hivyo kile ambacho kinashikiliwa na uongozi wa jeshi la Pakistan ndio kile kile ambacho ni kutafuta sababu za kutopigana.

Hivyo NDU imetoa aina hii ya kufikiri, ambayo ni, sababu za kuwa adui ni mwenye nguvu zaidi huhalalisha kutochukuwa hatua, kinyume na kutafuta sababu za kufanya wajibu wao? Mchambuzi mkuu mmoja wa masuala ya Ulinzi ameelezea “…China na Pakistan ni maadui wa wazi, Kashmir haiko na sisi, jeshi letu sio imara, majirani zetu wengi wako dhidi yetu, uchumi wetu unadidimia, tumekosa teknolojia, mizozo ya ndani si yenye kupungua … je nimeacha kitu chochote!” [2]. Kwa nini uongozi uliopata mafunzo wa NDU hauyaoni maelezo haya, ambayo ni ncha tu ya jiwe la barafu?

Haimalizikii hapa. Hadithi inayofuata ni kuwa watu wa Kashmir ni watazamaji tu na kwamba inawezekana wasiweze kuliunga mkono jeshi la Pakistan pindi likianzisha mashambulizi. Unafiki wa wale wanaoafiki hadithi hizi wanashawishiwa na Shaytan tu. Kwa zaidi ya miaka 30, kumekuwa na zaidi ya wanajeshi 700,000 wa India wakiwakandamiza zaidi ya Waislamu milioni 8 wa Kashmir. Kama Waislamu wa Kashmir ni walegevu, kwa nini kumehitajika jeshi la India kuweka askari 700,000, wakaongezeka kufikia zaidi ya 800,000 baada ya Agosti 5, 2019? Zaidi ya hayo, kwa kiasi cha mwaka mmoja kutokea tukio la Agosti 5, 2019, jeshi la India halikupunguzwa, na amri ya kidhalimu ya kutotoka nje haijaondoshwa. Kama ingekuwa hakuna ngome ya uungaji mkono katika Kashmir kwa ajili ya Pakistan, kwa nini jeshi la Pakistan limeunga mkono mapambano ya silaha ya Wakashmir kwa zaidi ya kipindi cha kutokea 1985 hadi 1999?

Katika mahojiano yote haya ya mazungumzo ya mjadala yaliopangwa vizuri ambapo wale wanaoitwa wachambuzi wa masuala ya ulinzi hutakiwa kuhalalisha msimamo wa jeshi la Pakistan, huweza kuwa ni kutoka jamii ya wasomi (intelligentsia) waletwe mbele badala yake kujibu swali la kwa nini makundi kama Lashkar Taiyaba na Jaish-e-Muhammad walitumika kuunga mkono uasi wa Kashmir katika kipindi cha 1985 hadi 1999.

Wakati hadithi hizo zikiwa zimejadiliwa kiakili, mtu anapaswa kushangaa kuhusu akili za wale waliozitoa. Kwa upande mwengine, inaibua swali la kuwa je kwa kweli wao hawajimudu. Zingatia kuhusu Jenerali Bajwa. Ametoa msaada wote wa lazima kwa wauwaji wa uchumi wa Pakistan, Dkt. Reza Baqir na Dkt. Hafidh Shaikh, kutekeleza mipango ya IMF, baada tu ya hapo mwaka mmoja baadaye (nchi) ikakabiliana na hali ambapo malipo ya deni yanayohusiana na IMF yameiacha hazina tupu  ikikosa malipo ya mishahara [3] baada ya malipo ya deni na matakwa ya jeshi kutekelezwa.

Hivyo tunaweza kuyaamini maamuzi ya mtu juu ya vita na India, wakati hana hata uwezo wa kufahamu matokeo ya mipango ya IMF anayoitekeleza? Kwa upande mwengine, inaibua swali la utiifu wao kwa Waislamu wa Pakistan, ambao kodi zao zinalipa mishahara yao. Kama uongozi wa kijeshi wa Pakistan hauna nia ya kupigana, lazima uwe na ujasiri wa kuelezea hilo, kuliko kutumia muda na nguvu kuzusha hadithi zisizo na maana. Kile kinachokuja akilini ni kama Mayahudi walivyoelezewa katika Surah Al-Baqara walipoamrishwa kuchinja ng'ombe. Mayahudi hawakuwa na nia ya kumchinja ng'ombe na wakaficha nia zao nyuma ya maswali yasio na msingi. Vivyo hivyo, uongozi huu hauna nia ya kupigana kwa ajili ya Kashmir au kwa ajili ya njia nyengine yoyote ya Uislamu na wanajificha nyuma ya masimulizi ya kupumbaza.

Kutokana na mtazamo wa Uislamu, hili ni la kutegemewa kutoka kwa wale wanaovunja wazi wazi Hukmu za Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) ametuonya wazi juu ya kuwafanya makafiri kuwa marafiki na wasiri wa ndani,

  [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ]

Enyi Mlioamini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasiokuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayokudhuruni.” [Surah Al-Imran 3:118]. Wale wasio na aibu ya kukiuka sheria za Mwenyezi Mungu (swt) hawatokuwa na aibu katika kuifanya rafiki Amerika na washirika wake ikiwemo India, kutafuta hukumu ya Umoja wa Mataifa, kuzawadia uchumi kwa IMF na hawatosita kuiuza Kashmir. Hivyo, tunapaswa kukataa simulizi zao. Sio tu kwa Kashmir lakini kwa kila kitu kwa msingi kuwa simulizi hizo ni kutoka kwa wale ambao kwa hiari na kwa kuendelea wanakiuka sheria za Mwenyezi Mungu (swt), na hivyo kukosekana wema katika fikra zao.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Khalid Salahudin – Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 19 Novemba 2020 22:32

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu