Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wanaadamu Hawawezi Tena Kuvumilia Mzigo Wa Urasilimali

Simamisheni Uislamu kwa Ajili ya Faraja Yao

Kiulimwengu na kindani nchini Pakistan, ni wazi kuwa Urasilimali upo katika mgogoro mbaya sana. Hata kabla ya mripuko wa maradhi ya Korona (Covid 19), mdororo wa kiuchumi ulikuwa wazi. Kote ulimwenguni, huduma za dharura za afya ya ummah zilikuwa mbovu na kuchukuliwa kama ni sehemu ya kinga kwa mdororo huo.

Hata hivyo, kimsingi, mrundikano mkubwa wa mali katika mikono ya tabaka la warasilimali wa Kimagharibi kwa sasa hauwezi kuvumilika, kwa watu wa Magharibi na kwa wengine Ulimwenguni. Hata katika kipindi cha mgogoro, utajiri wa mabilionea nchini Amerika umeongezeka kwa kiwango cha mamia ya mabilioni ya dolari. Mali za dhamana ni kwa kiwango cha trilioni za dolari ambazo kwa kawaida hunufaisha tabaka teule la warasilimali pekee. Hali hii, huku nchi kote duniani zinayumba chini ya hatua ngumu za kujibana, mzigo wa kupanda kwa kodi, kuongezeka kwa deni, kuvunjika kwa biashara, kuongezeka kwa ukosefu wa ajira na kutapakaa kwa kasi kwa umasikini.

Kwa upande wa hali ya ndani ya nchi, uchumi ukiwa unategemea zaidi juu ya uuzaji nje wa bidhaa na utumaji wa fedha kutoka nje na kiwango kikubwa cha bidhaa za nje zinazoagizwa. Pakistan imeathirika kutokana na mdororo wa uchumi wa kiulimwengu. Ama kwa upande wa mripuko wa maradhi, ufungiwaji ndani ya majumba umeongeza mdororo wa uchumi, kukiwa na uangukaji wa biashara nyingi, kuanguka kwa mapato na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira.

Hata hivyo, kimsingi, urundikaji wa mali wa kupangwa katika mikono ya tabaka la mabepari wa Kimagharibi na washirika wao wa ndani uko hai na kunawiri. Moja ya vyombo vyake muhimu kwa deni linalo ongezeka la Pakistan ni malipo ya riba. Kwa hivi sasa malipo ya riba ni rupia trilioni tatu za bajeti ambayo jumla ni ya trilioni saba. Kiwango cha riba cha mwaka jana kiliongezeka na kuwa ni miongoni mwa viwango vya juu zaidi vya marejesho ya faida kutokana na vitega uchumi kwa ulimwengu katika deni la Pakistan kwa wakopeshaji wa kimataifa na wa ndani. Mwaka huu ili kuwarahisishia tabaka la mabepari, deni hilo limeruhusiwa kubadilika thamani kupitia soko la hisa. Ili kuweza kulipa madeni haya, lengo la kiwango cha kodi mwaka huu ni rupia trilioni tano, kimeongezeka kutoka trilioni moja mwaka jana, likiwa lengo la IMF ni kuongezwa kodi kwa kila mwaka hadi ifikie rupia trilioni kumi mwaka 2024/2025.

Kiulimwengu na ndani ya nchi kuendelezwa kwa Ubepari hivi sasa hakukubaliki. Kile ambacho mwanzoni kikionyeshwa kama ni fikra bora ya kuigwa ya kiuchumi kwa ulimwengu hivi sasa inaendelea kuzingatiwa kuwa ni ndoto tu. Uislamu ukiwa na mtazamo wake wa kipekee wa kiuchumi katika mgawanyo wa mali, badala ya kuirundika, hivi sasa ni chaguo lisiloepukika. Ukomeshaji wake wa vyombo vya kibepari vya ukusanyaji wa utajiri, kama vile ufadhili uliojengwa juu ya msingi wa riba, umiliki binafsi wa nishati na madini na miundo ya kampuni za hisa, utapelekea faraja kubwa kwa dunia ambayo hivi sasa inateseka chini ya mizigo ya mfumo wa Kibepari. 

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Musab Umair – Pakistan

#كورونا        |        #Covid19             |       #Korona

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 29 Julai 2020 16:20

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu