Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Agosti 5 na Siasa za Vita Ndani ya Kashmir Iliokaliwa

Tarehe 5 Agosti 2020 inaadhimisha mwaka wa kwanza baada ya kutenguliwa Kifungu cha 370 cha katiba ya India, ambapo Kashmir iliunganishwa rasmi na Muungano wa India. Ukombozi wa Kashmir umeleta taswira ya kupendeza kwa muumini hodari na mchunguzi. Cha kulengwa ni namna ya fikra ya Faradhi (Wajibu) inavyomsukuma muumini kutafuta suluhisho kwa matatizo ambayo kwa muonekano wa juu juu haimkiniki kuwezekana. Mwenyezi Mungu (swt) amesema katika Quran,

لَا يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

“Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri iwezavyo” [TMQ 2:286]. Na utekelezaji wa Hukmu za Jihad ni lazima ziwezekane, vyenginevyo Mwenyezi Mungu (swt) asingezifanya kuwa ni wajibu (Fardhi).

Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha,

وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ

“Na wauweni popote muwakutapo, na muwatoe popote walipokutoweni” [Surah al-Baqarah 2:191]. Ina maana kuwa nguvu zetu lazima tuzitumie katika kupigana na maadui, kama nguvu zao wanavyozitumia kwa kupigana nasi, na kuwafukuza kutoka katika maeneo waliyotutoa. Mwenyzi Mungu (swt) amesema,

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ قَاتِلُواْ الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللّهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ)

“Enyi mlioamini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu, na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha Mungu” [Surah at-Tawbah 9: 123]. Na Mtume (saw) ametuonya,

«مَا تَرَكَ قَوْمٌ الْجِهَادَ إلاّ ذُلّوا»

“Watu hawatoacha Jihad isipokuwa watadhalilishwa.” [Ahmad].

Mtume (saw) amesema,

«وَالْجِهَادُ مَاضٍ مُنْذُ بَعَثَنِيَ اللَّهُ إِلَى أَنْ يُقَاتِلَ آخِرُ أُمَّتِي الدَّجَّالَ لاَ يُبْطِلُهُ جَوْرُ جَائِرٍ وَلاَ عَدْلُ عَادِلٍ، وَالإِيمَانُ بِالأَقْدَارِ»

“Jihad ni yenye kuendelea tokea Mwenyezi Mungu aliponipa Utume hadi watakapopigana wa mwisho wa Ummah wangu na Dajjal. Hatoitengulia na udhalimu wa (mtawala) dhalimu wala uadilifu wa (mtawala) muadilifu, na imani kwa qadar.” [Abu Dawud]

Dalili hizi na nyengine nyingi zinaweka wazi kwa muumini kuwa sheria za Mwenyezi Mungu (swt) lazima zitekelezwe. Mchakato wa fikra unaotakikana nazo na dalili nyengine nyingi ni kuwa Hukmu za Mwenyezi Mungu lazima zisimamishwe. Hii hutoa ufafanuzi wa matakwa ya kutafuta suluhisho. Kwa hiyo, vita na matayarisho kuelekea ukombozi ni lazima. Mazungumzo juu ya vita hufungua maswali mengi juu ya uwezekano wa kushinda katika vita. Wakati ushindi na kushindwa ni kutokana na Mwenyezi Mungu (swt), tukiwa ni waumini tunatakiwa kuangalia matokeo chanya, nayo ni ushindi. Hebu tuzingatie hili katika suala la hatua zilizopo katika kuikomboa Kashmir.

Uwepo wa silaha za nyuklia kwa pande zote mbili humaanisha kuwa vita vitakwenda katika njia ya kawaida, kwa kuwa hatua ya utumiaji wa silaha za nyuklia utapelekea moja kwa moja katika hakikisho la uangamivu kwa wote (MAD). Ulinganishaji katika kutumika njia za kikawaida hautoi upendeleo kwa Pakistan, angalau kwenye karatasi, kwa kuwa India imeizidi Pakistan kwa takriban mara tatu katika pande zote hizo za kawaida.

Uwanja wa vita hauna mipaka, hivyo ni kipi kinachoizuia Pakistan kutoshajiisha uasi wa kisilaha katika Kashmir, sambamba na jeshi la Pakistan kutangaza vita Kashmir? Kati ya watu wote milioni kumi na mbili wa Kashmir, milioni tisa ni Waislamu, wengi wao hivi sasa ni wapinzani wa India moja kwa moja. Hivyo mashambulizi ya udunguaji, IED na uvamizi hivi sasa ni ya uwezekano wa wazi katika Kashmir, ambapo vikosi vya India vitalazimika kukabiliana nayo. Hivyo hata kama India itaweka vikosi vya askari milioni moja Kashmir, hawatoweza kukandamiza uasi, kama Waislamu hawa wataungwa mkono kijeshi na kwa silaha. Hadi hivi leo, Waislamu wa Kashmir iliokaliwa kimabavu hawajaondoa matumaini katika “Kashmir banagay Pakistan” (Kashmir itakuwa Pakistan) na bado wanawafunika mashahidi wao kwa bendera ya Pakistan. Amerika imejifunza funzo kubwa Iraq na Afghanistan ambapo waasi walioleleka nyumbani inakuwa vigumu kuwadhibiti. Kama Amerika haikuweza kufanikiwa katika maeneo haya, basi vipi India itaweza katika Kashmir?

Kwa mtazamo wa India, ni kuwa itaweza kuongeza idadi ya vikosi Kashmir. Hata hivyo, hali ya ndani ya India sio tulivu, hata ikilinganishwa na ya Pakistan. Kuna idadi kubwa sana ya uasi kote nchini India. Kuna kisiwa kuwepo na takriban mashirika makubwa 68, yanayo daiwa kuwa ni makundi ya kigaidi, ndani ya India. Kiwango hicho cha idadi na wigo kinaweza kujadiliwa, lakini kisichoweza kujadiliwa ni uwepo wake na uzito wa kuyakabili kupitia operesheni za kijeshi. Hivyo India inaweza kupeleka vikosi kutoka eneo moja kwenda jengine, lakini kisha mjadala utahama kutoka mawanda ya kijeshi hadi ya kisiasa.

Kuna hasara za kisiasa kwa uhamishaji wa vikosi kutoka sehemu moja kwenda nyengine, hata katika mzozo mfupi. Kuhamisha askari kutokea kwa waasi wa Naxalite hadi Kashmir kunaweza kuongeza nguvu kwa harakati ya waasi wa Naxalite, watakaoiona kuwa hii ndio fursa ya kutangaza kujitenga. Hivyo, sasa uamuzi utakuwa na athari pana ima kuwepo na mapatano ya kisiasa pamoja na harakati za waasi, ambapo itamaanisha kuachia nafasi ya kisiasa, itakayo dhoofisha nafasi ya India au kutokuwepo na hatua ya kijeshi ya kusafirisha vikosi. Hivyo, katika hali ya ndani, India itazidisha na kujifunga kwa matatizo yake yenyewe ya ndani. Hii ni mbali na kiasi cha Waislamu milioni mia mbili wa India ambapo serikali ya BJP imeamua kuwatenga.

Kwa upande wa nje ya nchi, katika mipaka yake, India vile vile imeendelea kukabiliwa na kiwango kikubwa cha mzozo wa mipaka, ikiwemo mzozo wake na China. Haya ni maeneo ambapo kwa zaidi ya muongo mmoja, vikosi vya China na India vimekuwa vikipambana. Askari wa India waliopo hapo hawatoweza kuondoshwa. Kuna mazingatio ya kimkakati hapa. Mzozo wa hivi karibuni wa Uchina na India katika bonde la Galwan ni muendelezo wa mapambano mapana ya kimkakati baina ya Amerika na China, na hivyo kuufanya mpaka na India kuwa ni sehemu ya eneo nyeti la maslahi ya China. Hii inamaanisha kuwa China haitabakia tu kwenye mpaka na kudumisha uhasama, bali itakuwa na hamu ya kuidhoofisha na kuisukuma nyuma India.   

Mzozo huu una vipimo vyake wenyewe. Katika mwezi wa Juni 13, 2020, bunge la Nepal limekubaliana kwa pamoja kuibadilisha ramani ya nchi kulijumuisha eneo linalodaiwa na jirani yake upande wa kusini. India imeitaja hatua hiyo kuwa “isiyo kubalika” na kusema imekiuka maelewano ya kuwa mizozo ya mpaka itatatuliwa kupitia mazungumzo. Kipindi hiki ni murua kwa kuwa kinasadifiana na kuongezeka kwa uhasama baina ya India na China. Hivyo mzozo wa China na India katika bonde la Galwan umetokana na Nepal kuzingatia upya juu ya mipaka yake na India. Je India inayo afueni kwa kufikiria kuwa wengine hawatofanya hivyo hivyo endapo kutatokea vita Kashmir? 

Zingatia pia eneo la kistratejia la Chicken’s Neck, linalijulikana kwa barabara ya Siliguri, njia ya kutoka India kuelekea majimbo ya kaskazini mashariki. Eneo Jekundu (The red region) linalojulikana kwa jina la Doklam, ni sehemu ya bonde la Doklam. India imejaribu kuishawishi Bhutan, tokea 2018, kupeleka askari wengi zaidi katika eneo la mzozo la Doklam. Kama China italichukua eneo hili itaweza kudhibiti mwenendo wa safari za barabara ya Siliguri, ambapo itazuia usambazaji kwa majimbo ya Seven Sisters, au kuzuia jeshi la India kutokana na ugandamizaji wa ushawishi wa uasi wa ndani.

Kutokana na uhasama wa sasa, endapo China itachukua msimamo wa shari kwa Bhutan kwa badali ya usalama na usaidizi, je Bhutan itaiunga mkono India au itarudi nyuma chini ya shinikizo na kuifanya barabara ya Siliguri kuwa katika mazingira ya kushambuliwa na China?

Hii ni mifano hai ya namna ambavyo nchi ya tatu imeamua kupatiliza fursa ya makabiliano ya China na India, kwa ajili ya miundo ya eneo lake wenyewe. Hivyo kama kutakuwa na mzozo mpana baina ya China na India, je nchi nyengine pia zitazusha uhasama na India? Kwa upande wa kisiasa, ni suala la kinga ya bahati nasibu. Hivyo huku Japan na Korea Kusini zikiwa zimeshirikiana na Amerika, zingali zinadumisha mahusiano na Wachina kwa sababu Amerika imekuwepo tu kwa takriban miaka 200 iliopita pekee, lakini China imekuwa jirani yao kwa zaidi ya miaka 4000 iliopita.

Wang Xianfeng, afisa habari wa ujumbe wa China jijini Islamabad, mnamo 11 Juni 2020 alituma ujumbe wa twitter: “Vitendo vya India vya upande mmoja vya kuibadilisha hali halisi ya Kashmir na kuendelea kuongeza uhasama wa kieneo vimeleta changamoto kwa mamlaka ya China na Pakistan na kufanya mahusiano ya India na Pakistan, na ya China na India kuwa magumu zaidi” na kisha mara moja akauondoa ujumbe huo wa twitter siku nne baadaye. Hii ni dalili ya jaribio la China kuirubuni Pakistan kuingia katika majadiliano ya Kashmir katika msuguano wa sasa. Hii ni sawa na operesheni iliopita ya Amerika katika Abbotabad, ambapo Uchina ilitoa tamko kuwa shambulizi kwa Pakistan ni shambulizi kwa China. Uchina inaiona Pakistan kuwa ni nguvu ya uzani dhidi ya Wahindi na Amerika. Hivyo Uchina inapendekeza nini kupitia ujumbe huu wa twitter? Katika vita vya 1962, Balozi wa Uchina jijini Islamabad alimtembelea Jenerali Ayub Khan na kumuuliza kwa nini bado hajaitumia fursa ya hali iliyopo kwa kuichukua Kashmir. Uwiano ni wa kushangaza na kulazimisha.

Hivyo matumizi halisi ya uchambuzi wa kisiasa ni kusaidia kuelezea sera zinazoweza kutumika kuwakabili maadui wa nje. Ndani ya pazia hili la nyuma, kama Pakistan ingelitangaza vita dhidi ya Kashmir, mazingatio yote hapo juu yangepaswa kuzingatiwa na Wahindi katika majibu yao.  Hivyo kwa uhalisia, vipi India itaweza kukabiliana na changamoto hii? Tatizo la China na India sio ghasia za mpaka, bali ni India kuwa katika mrengo wa Amerika, ambayo inatumia eneo lote kuidhibiti Uchina. Uwezekano wa China kuingia katika vita vyenye kikomo katika eneo lolote la maeneo haya kwa wakati mmoja, na Pakistan kuingia Kashmir, kungeweza kumaliza mchezo kwa India. Uchina ilivilenga vita vya Indo China mwaka 1962 kwenda sambamba na mzozo wa makombora ya Cuba. Nyaraka zilizotolea kutokea kipindi hicho zilionyesha hofu ya Amerika na India kwa Pakistan kama ingeliingia vitani. Aliyekuwa balozi wa Amerika nchini India alielezea "Jinamizi la mashambulizi ya pamoja ya Pakistan na China, huku kukiwa na uwezekano wa kushindwa, kuporomoka na hata machafuko nchini India, lilikuwa likinisumbua akili yangu mno". Hivi leo, Uchina ni yenye nguvu zaidi, na Amerika si tu ni dhaifu, bali yenye kushughulishwa mno.

Mjadala wa hapo juu unaibua swali msingi, endapo vita vitatokea, ni ipi sera ya India? India haina sera zaidi ya Amerika, na Amerika sio sera ya kuifaidisha. Trump yuko katika mwaka wa uchaguzi, na anakumbana na matatizo mengi. Uchumi ambao kwa kawaida ndio suala nyeti katika uchaguzi wa Marekani, umevurugika, na Trump ameangukia katika usaliti wa kiwango kikubwa, usalama wa taifa, baada ya vuguvugu la kutaka maisha ya watu weusi yazingatiwe (Black Lives Matter). Hivyo mbali na kutoa msaada sawa wa kisiasa na kidiplomasia, ni nini jengine inaloweza kufanya?

Pindi Urusi ilipoiunganisha Crimea, Amerika ilisimama na kuangalia na kuweka vikwazo tu, kimsingi kwa sababu eneo hili halikuwa ni sehemu ya maslahi nyeti ya Amerika. Hivyo je Kashmir na uhasama na Uchina kweli yako ndani eneo muhimu la maslahi ya Amerika? Wakati maisha ya watu weusi nchini Amerika hayazingatiwi, je maisha ya wekundu, walio umbali wa maelfu ya maili yatazingatiwa?

Uhalisia unaonyesha kuwa vita ni vyenye uwezekano wa kutokea, lakini bado uongozi wetu fisidifu wa kiraia na kijeshi hawalitekelezi hili. Mjadala wa hapo juu unawahusu hasa wale wanaouamini Uislamu kama suluhisho na wako tayari kujitoa mhanga kufikia malengo ya Uislamu. Hata hivyo, uongozi wa sasa umefilisika katika kufikiri, kwa Uislamu au vyenginevyo, kiasi cha kutozingatia hata kiwango kidogo cha vita.

Kiwango kidogo cha vita sasa dhidi ya Kashmir vitaweza kutatua matatizo mengi kwa serikali ya sasa, hata kwa mtazamo finyo, wa kitaifa. Kwanza, kusinyaa kwa bahati nzuri za jeshi kunaweza kupanda juu muda wote. Pili, migawanyiko ya sasa katika majukwaa ya kisiasa inaweza kutoweka kwa kuwa yeyote atakaye jaribu kupinga vita katika Kashmir atachukuliwa kuwa ni mhaini. Tatu, uchumi utapata msukumo kwani inajulikana wazi kuwa suluhisho bora kwa mdororo ni vita. Hata hivyo, viongozi wa sasa wamefilisika kutokana na kufikiri kwa uhuru ambapo hawawezi kufikiri kwa namna hii. Ukweli ni kuwa sera wanazozifuata ni za mabwana zao, wakoloni, na wanazitekeleza kwa maslahi yao binafsi. Hawakuvifanya vita kuwa haramu kwao binafsi pekee, wameviharamisha kwa waasi wa Kashmir kwa miongo mingi. Kwa maagizo ya wakoloni, wameweka msimamo kuwa uasi wa Kashmir ni “ugaidi” na wanafanya kazi kuumaliza, na kuipa Dola ya Kibaniani utulivu wanaohitaji mno.

Suluhisho la Kashmir ni Jihad na hili haliwezi kutokea kupitia viongozi fisidifu unaosaka suluhisho katika fikra za Kikafiri zinazozaa tatizo. Ni kupitia Khilafah pekee kwa Njia ya Utume, ambayo ina ikhlasi katika kutekeleza Uislamu na inayojali mazito ya Ummah, sio tu Kashmir itakayo kombolewa pekee, bali ulimwengu wote wa Waislamu kutokana na mfumo huu fisidifu wa kikafiri.

Imeandikwa Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Khalid Salahuddin – Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu