Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Dola za Kitaifa: Ni Ngao ya Uovu

Vita vya dunia vimetengeneza maafa makubwa kwenye mfumo wa Kibepari; himaya zimevunjika na idadi ya dola za kitaifa imeongezeka kwa kasi. Uongezekaji huu umesifiwa kuwa ni ushindi kwa watu kote duniani; tulikuwa hatupo tena kwenye huruma ya mataifa ya Ulaya, lakini hatimaye tulipata haki zetu na tuliweza kujitawala kulingana na namna ilio bora kwetu. Mataifa katika Afrika, Asia, na Mashariki ya Kati yaliweza kuchagua watawala wao wenyewe. Hivyo, kwa nje walikuwa na uwezo wa kukwepa utawala wa Kimagharibi.

Yote haya yalitokea kwenye karne ya 20. Miaka iliofuata tokea kipindi hicho ilionyesha yote haya kuwa ni uongo. Kuibuka kwa dola za kitaifa hakukutusaidia – kumetudhuru, na imekuwa ni kama ngao ya mfumo wa Kimagharibi. Imeleta mgawanyiko katika jamii kote duniani, imeimarisha mivutano ilioachwa nyuma na sera ya wakoloni ya wagawe uwatawale. Hii imeiathiri kila jamii, kote katika ulimwengu wa Kiislamu na usio wa Kiislamu.

Matokeo yake ni kuwa tunaishi katika ulimwengu ambao watu kwa ujinga huamini kuwa wako huru kutokana na utawala wa Kimagharibi. Uhalisia wa nidhamu ya sasa ya kisiasa, na maamuzi yanayoibuka kutokana nayo, inaonyesha kuwa hilo liko mbali na ukweli.

Nguvu ya Waislamu katika Umoja

Nguvu kuu ya Waislamu muda wote imekuwa katika umoja wao. Mipaka haikuuvunja Ummah wa Kiislamu. Tuliungana katika fikra zetu, imani yetu kwa Mwenyezi Mungu na rasilimali zetu.

Wakoloni waliishambulia fikra yetu na walitugawa kwa kuukata Ummah wa Kiislamu katika mipaka ya dola za kitaifa, wakiwaweka watawala walioendelea kutuweka nyuma na kushajiisha utiifu kwa fikra ya utaifa kwa kiwango cha juu zaidi ya utiifu wetu na majukumu kwa Mwenyezi Mungu, sheria Zake na Ummah wa Waislamu. Kisha kuuweka Uislamu nyuma, lakini wakiuleta mbele katika hotuba na maneno wakati wanapoona ni maslahi kwao. Matokeo yake, hawako na haraka ya kukabili vitisho kwa Ummah wa Kiislamu na vitisho kwa Uislamu.

Mifano ya vitisho hivi na uhalisia tunaokabiliana nao ni mkubwa

- Machafuko ya sasa wanayokabiliana nayo Waislamu kote duniani, ima yawe katika maeneo ya vita kama Yemen na Syria, maeneo ya machafuko ya kikabila kama Myanmar na China, au nchi za Kimagharibi zinazofanya mashambulizi dhidi ya Waislamu kama tuonavyo katika mashambulizi dhidi ya wanawake Waislamu nchini Ufaransa.

- Kuna mashambulizi dhidi ya Uislamu, Ufaransa ikishajiisha matangazo ya karaha ya picha za Mtume (saw).

- Kisha kuna hali jumla ya Ummah wa Kiislamu, ulio na kiwango kinachoongezeka cha umasikini na kutokuwepo usawa kote duniani.

- Katika kila moja ya hali hizi, mipaka ya dola za kitaifa hutumika kama ni sababu ya kukosekana ufumbuzi wa matatizo. Mfumo wa kimataifa unaweka vikomo juu ya miitiko ya dola, kwa udhuru ya kuhakikisha kuwa dola kote duniani zitaweza kufanya kazi pamoja kwa uvumilivu na kuepuka vita. Lakini haya hayafanyiki kwa kuzingatia maslahi ya watu – bali hufanyika kuhakikisha kuwa nidhamu ya kiliberali inayolenga juu ya dola za kitaifa kuwa ndio chanzo cha nguvu, kwamba kinadhibitiwa.

Dola ya Kiislamu haina mipaka – na lengo lake kuu ni kuuhifadhi Uislamu na Ummah wa Kiislamu

Chini ya Dola ya Kiislamu, hakuna mipaka – Ummah wote wa Kiislamu umeunganishwa, kwa Khalifah mmoja anayeuhifadhi Uislamu na Ummah wa Waislamu, ukiwahakikishia kuwa haki zao zinatimizwa na mahitaji yao msingi yanatoshelezwa. Chini ya Khilafah, utakuta:

- Baytul Mal, yenye kusanya mali kutoka maeneo yote ya Khilafah na kuisambaza kule inakohitajika kuhakikisha kila raia anakidhiwa mahitaji yake.

- Jeshi la Waislamu, lenye kukabili kitisho chochote dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mtume wake au Ummah wa Waislamu.

- Khalifah, anayefuata sheria za Mwenyezi Mungu na kuunganisha majeshi duniani kote chini ya dola moja, kuwaongoza kuilinda heshima ya raia wa Khilafah.

Ili kuhakikisha kuwa hali inabadilika, ni kuwa hatugeukii juu ya taarifa tu na kuangalia ukatili ukifanyika kila leo, tunahitaji kubadilisha mfumo. Mabadiliko haya yanakusudiwa kuvunja dola za kitaifa na kusimamisha tena dola ya Kiislamu kwa njia ya Utume. Kama tunavyoona kutoka katika Hadithi mashuhuri ya Mtume (saw), wakati alipokataa takwa la Maquraysh kuendeleza utawala wao sambamba na utawala wa Kiislamu;

 «لَوْ وَضَعُوا الشَّمْسَ فِي يَمِينِي وَالْقَمَرَ فِي شِمَالِي عَلَى أَنْ أَتْرُكَ هَذَا الْأَمْرَ حَتَّى يُظْهِرَهُ اللَّهُ أَوْ أَهْلِكَ فِيهِ مَا تَرَكْتُهُ»

“Lau wataliweka jua katika mkono wangu wa kulia na mwezi katika mkono wangu wa kushoto ili niwachane na jambo hili, sitoachana nalo hadi Mwenyezi Mungu anifanye kuwa mshindi, au niangamie kwalo.”

Usifanye makosa – walinzi wa mfumo wa kiliberali wanalijua hili, na ndio tunashuhudia wanaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya Uislamu. Kuwafanya Waislamu na wasio Waislamu kuhofia fikra ya ‘Uislamu wa Kisiasa’. Wanafahamu kuwa dola ya Kiislamu itaporudi, itakuwa ndio mwisho wa mfumo wa sasa uliopo. Wanafahamu pia kuwa dola ya Kiislamu haitopata usaidizi wa Waislamu tu, bali itapata pia kutoka kwa wasiokuwa Waislamu, kwa kuwa ni sheria za Mwenyezi Mungu tu ambazo zinahakikisha kuwa kila raia wa Khilafah anaamiliwa kwa usawa na kupatiwa haki zake za msingi. Historia ina mifano mingi ya yote haya. Hivi sasa, watetezi wa mfumo wa Kimagharibi wanakhofu kuwa historia itajirejea tena baada ya wao kutumia karne nyingi bila kuchoka dhidi ya Uislamu na kuuvunja uaminifu wa watu kwake.

 «كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمْ الْأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لَا نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَتَكُونُ خُلَفَاءُ تَكْثُرُ»، قَالُوا فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: «فُوا بِبَيْعَةِ الْأَوَّلِ فَالْأَوَّلِ وَأَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ، فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ»

“Walikuwa Banu Israil wakisimamiwa siasa zao na Manabii wao, kila akifa Nabii mmoja anakuja mwengine, lakini hakuna Nabii baada yangu mimi, watakuwepo Makhalifah na watakuwa wengi", wakasema (Maswahaba) unatuamrisha nini? Mtume (saw) akasema: "Mpeni bay’ah (ahadi ya utiifu) mmoja baada ya mwengine na wapeni haki zao (kuwatii), hakika Mwenyezi Mungu atawauliza kuhusu majukumu aliyowakabidhi”. (Sahih Bukhari #3455)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Fatima Musab

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu