Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Njia ya Kufikiri Katika Uislamu

na Mambo Msingi ya Mtazamo wa Kiislamu

Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[وَلَكِنَّ اللَّهَ حَبَّبَ إِلَيْكُمُ الْإِيمَانَ وَزَيَّنَهُ فِي قُلُوبِكُمْ وَكَرَّهَ إِلَيْكُمُ الْكُفْرَ وَالْفُسُوقَ وَالْعِصْيَانَ أُوْلَئِكَ هُمُ الرَّاشِدُونَ]

“Lakini Mwenyezi Mungu amekupendezeeni Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na amekufanyeni muuchukie ukafiri, na upotovu na uasi. Hao ndio walioongoka.”  [Al-Hujurat: 7].

Hii ndio namna Mwenyezi Mungu Mtukufu amemuelezea Muumini. Hata hivyo, tunashuhudia baadhi ya Waislamu wanapendezwa na ukafiri, kutokuwa na utii au madhambi badala ya kuyaepuka na kuyazingatia kuwa ni machukizo. Wanazingatia nguruwe kuwa ni haram (chukizo) wakati huo huo huchukulia matumizi ya riba katika biashara zao kuwa ni muhimu. Wakati Uislamu umeielezea riba kuwa ni kutangaza vita dhidi ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Demokrasia ni ukafiri na ushirikina…, lakini bado kuna Waislamu wanaotoa mamlaka kwa mwanaadamu na kuyasifia. Usekula ni ukafiri na kupingana na Mwenyezi Mungu (swt), lakini bado kuna Waislamu wanaotaka kuyaacha maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) katika masuala ya kimaisha. Kipimo cha matendo kinapaswa kuwa ni Halali na Haramu, lakini baadhi huyaelekeza kwenye manufaa na hasara. Licha ya kuwa Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha kuwapuuza makafiri na washirikina, lakini kuna wanaolingania mapatano na muungano baina yao. Kuna mifano mingi ya aina hii…

Kwa vipi inawezekana kuwa Waislamu wanaingia katika mgongano huo? Hivyo; kufikiri ni suala lenye umuhimu usiopingika kwenye maisha ya mwanaadamu. Uwezo wa kufikiri katika namna sahihi ndio unaomtafautisha mwanaadamu na mnyama. Kufikiri ni mchakato wa kuhukumu kuhusiana na vitu na matukio kupitia utumiaji wa akili. Mtu hunyanyuka kutoka kwenye hadhi ya mnyama kupitia uwezo wake wa kutenda kwa mujibu wa maamuzi aliyoyafikia baada ya kufikiri. Kinyume chake; mtu asiyefikiri, hutenda kwa mujibu wa matamanio na matashi yake, kama mnyama. Huu ndio ukweli ambao Mwenyezi Mungu (swt) anauelezea katika Quran.

[أَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَهَهُ هَوَاهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيْهِ وَكِيلاً * أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلاً]

“Je umemuona aliyeyafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake? Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake? Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanaelewa? Hao hawakuwa ila ni kama nyama hoa tu, bali wao wamepotea zaidi njia.”  [Al-Furqan: 43-44].

Aya hii kimsingi inahimiza umuhimu wa kufikiri, kufikiri kiakili. Kwa upande wa Waislamu; Muislamu sio mtu wa kawaida tu. Ni yule, ambaye amefanya makubaliano na Mola wake kwa kutamka LA ILAHA ILLALLAH, MUHAMMAD AR-RASULULLAH. Neno “illah” maana yake, “Wewe pekee ndiYe ninayekuabudu, ninaye kunyenyekea, na ninaishi kulingana na kile Ulichokiteremsha, na ndicho ninachokiamini – Quran Yako na njia ya Ujumbe Wako.” Muislamu ni mtu, anayesalimisha fikra zake, matamanio yake, hisia na matendo yake kwa Bwana Mmoja. kwa hivyo, shakhsia yake inaitwa shakhsia ya Kiislamu, tabia za Kiislamu. Na hii ndio shakhsia ambayo Muislamu anatakiwa ashikamane nayo.

Shakhsia ya mtu inajengwa juu ya ufahamu wake na tabia, ambayo hujengwa kwa mujibu wa fikra maalum, wakati tabia zake ni matendo yanayoendeshwa na mielekeo yake, yaani silka na mahitaji ya kimwili.

Ni nidhamu ya kufikiri ambayo hutafsiri mema na maovu, yalio sahihi na yasio sahihi, yenye kupendeza na yasio pendeza… Ni nidhamu ya kufikiri ilio thabiti ambayo inaongoza mielekeo ya mtu kwenye tabia maalum, na inayounda hisia zake, kama kupenda na kuchukia, kuridhika na kutoridhika. Uthabiti huu ndio unaojenga shakhsia.

Ili tuweze kuiendeleza shakhsia ya Kiislamu, akili ya mtu lazima ijengwe juu ya Aqida ya Kiislamu. Hivyo kwa Muislamu, ni Bwana wake na Muumba wake, ndiye anayefafanua mema na mabaya, yalio sahihi na ya makosa, yenye kuridhiwa na yasioridhiwa.

Hivyo fikra hizi pia zinatengeneza hisia za Waislamu na matashi, ambayo yanapelekea katika njia maalum ya kutenda matendo, yaani kutenda matendo mazuri, na hatimaye kuipata shakhsia ya Kiislamu. Kwa hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) ametueleza namna ya akili ya Muislamu na mielekeo yake inapaswa iwe:

«لَا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَوَاهُ تَبَعاً لِمَا جِئْتُ بِهِ»

“Haamini mmoja wenu mpaka matamanio yake yafuate yale niliokuja nayo mimi” [Bukhari, Muslim]

Zaidi ya hayo, Mwenyezi Mungu (swt) anahitaji kutoka kwa Waumini kuhakikisha uthabiti katika maneno yao na matendo:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ * كَبُرَ مَقْتاً عِندَ اللَّهِ أَن تَقُولُو امَا لَا تَفْعَلُونَ]

“Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyo yatenda? Yanachukiza vikubwa mno kwa Mwenyezi Mungu kuwa mnasema msiyo yatenda.” [As-Saf: 2-3].

Bwana wetu ametuonya katika aya zifuatazo kwenda kinyume na fikra na mielekeo yetu:

[أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ أَفَلاَ تَعْقِلُونَ]

“Je Mnawaamrisha watu mema na mnajisahau nafsi zenu, na hali nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je, hamzingatii”? [al-Baqarah: 44].

Hivyo tunaona kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametusisitiza na kutuamuru kuwa na shakhsia ya Kiislamu ilio thabiti. Ili tuwe na shakhsia ya Kiislamu ilio thabiti, inahitajia kuifanya Aqida ya Kiislamu kuwa ndio msingi wa kufikiri. Na ili tuweze kutekeleza kitendo cha kufikiri, inatakiwa kutekeleza njia yake. Kwa hivyo shakhsia ya Kiislamu inaweza tu kuundwa  kupitia kujengwa juu ya Aqida ya Kiislamu, yaani kuifanya ndio msingi wa akili na mielekeo, yaani kuichukua Quran, Sunnah na Ijmaa ya Masahaba (ra) kuwa ndio njia ya kufikiri.

Hii ina maana, kuwa kabla ya kuamua juu ya hali au jambo, au kabla ya kuamua juu ya matendo yetu…

  1. Tunahitaji kufahamu uhalisia wa hali au suala kwa undani.
  2. Kisha tunahitaji kupata dalili zinazohusiana za Sharia juu ya jambo hilo.
  3. Tunahitaji kuangalia dalili za Kisharia, Quran na Sunnah, kwa ujumla wake.
  4. Tunatakiwa kuichukua hukmu ya Kisharia iliovuliwa kwa bidii na kutenda kwa mujibu wake.

Hii ndio namna ya kujenga utambulishao wa Kiislamu. Hii itatoa sura ya kimsingi ya akili hii. Suala la mwanzo ni kuweka ufahamu wa kuwa utumwa uwe kwa Mwenyezi Mungu ambao unaongezeka kwa huruma na utii. Jambo la pili ni kuitafuta hukumu ya Kisharia kabla ya kutenda, bila kubagua, kama ilivyoelezwa katika aya inayofuata:

    [وَلاَ تَقْفُ مَالَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولـئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْؤُولاً]

“Wala usiyafuate usio na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa.” [Al-Isra: 36].

Jambo la tatu ni kutathmini matokeo ya jambo kwa mtazamo wa Maisha ya Akhera. Hii ina maana, ni lazima kabisa kuamua kwa mujibu wa kipimo cha nini kinaruhusiwa na nini hakiruhusiwi. Hakika, Mwenyezi Mungu (swt) ameagiza:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُو اقَوْلاً سَدِيداً * يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَمَن يُطِعْ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزاً عَظِيماً]

“Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa. Apate kukutengezeeni vitendo vyenu na akusameheni madhambi yenu. Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa.” [Al-Ahzab: 70-71].

Alhamdulillahi Rabbil ‘Alamiin.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Aynur Yazar

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 14 Disemba 2020 17:27

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu