Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kila Janga ni Fursa

Mtafaruku wa kimataifa umefikia kileleni kwa sababu ya vitendo vya kihalifu na kigaidi vinavyotendwa na umbile ovu la Kiyahudi dhidi ya kipenzi chetu Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Umbile ovu linaendelea kuwaua kaka na dada zetu Waislamu na kuipora Ardhi yetu Iliyobarikiwa ya Palestina! Inatenda uhalifu huo kwa ushirikiano na ridhaa za watawala vibaraka wa kikoloni wa eneo wakiongozwa na Abdel Fattah al-Sisi (Egypt), Abdullah II bin al-Hussein (Jordan), Bashar al-Assad (Syria), Mahmoud Abbas (Palestinian Authority), Muhammad bin Salman (Saudi Arabia), Recep Tayyip Erdogan (Türkiye) miongoni mwa watawala wengine ‘Waislamu’ vibaraka wa kikoloni.

Umbile la Kiyahudi lipo kama kivuli cha watawala ‘Waislamu’ vibaraka wa kikoloni wanaolizunguka na ambao wanaabudu Washington na London. Limeundwa na utawala wa Uingereza na hivi sasa linamakinishwa na utawala wa Kiamerika. Msingi wake wa nguvu za kijeshi umekitwa juu ya propaganda, ambao kiuhalisia ni kama mtandao wa buibui. Uthibitisho ulikuwa ni mnamo Jumapili 8 Oktoba 2023 pale ambapo Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alipotangaza kwamba ameagiza meli za kijeshi za Marekani, zikijumuisha zinazobeba ndege na ndege za ziada, kusongea karibu mashariki ya Mediterranean ili kujibu mashambulizi ya kushtukiza na kutoka kila pembe yaliyotekelezwa na Hamas dhidi ya ‘Israel.’ [CBS News, 9/10/2023]. Afisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza ilitangaza mnamo Alhamisi 12 Oktoba 2023 kwamba Uingereza inazituma meli za kijeshi za Kifalme, helikopta na ndege za kijasusi mashariki ya Mediterranean ili kuinusuru ‘Israel’ na kuiimarisha kieneo. [Reuters, 12/10/2023].

Ili kufichua zaidi udhaifu wa umbile la Kiyahudi ni Rais Biden kulizuru mnamo Jumatano 18 Oktoba 2023 na kulihakikishia uungwaji mkono thabiti na kuliahidi msaada zaidi wa kijeshi na mengine yadharura. Kwa kuongezea, Waziri Mkuu Rishi Sunak alilizuru mnamo Alhamisi 19 Oktoba 2023 na kutoa ahadi ya kulinusuru na kusimama nalo kidete dhidi ya maadui zake. Na kabla ya ziara za Biden na Sunak, mawaziri wao wa kidiplomasia kwa maana Antony Blinken (US) na James Cleverly (UK) walisafiri mwanzo ili kuandaa mazingira kwa ajili ya ziara za viongozi wao.

Hakika, kama ilivyosemwa, ‘Katika kila janga, huwepo fursa kubwa.’ Janga linaloendelea lina fursa zifuatazo punde tutakapoamka na kuitikia mwito wa Mwenyezi Mungu (swt): ﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ “Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Fursa za muda ni:

Kwanza, lazima tuchangamke na kuwalingania waziwazi kaka zetu Waislamu walioko katika majeshi ya Waislamu kuzinduka na kujibu vilio na machozi ya ndugu zetu Waislamu ndani ya Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kama agizo kutoka Mwenyezi Mungu (swt): ﴿وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Anfal: 72]. ﴿إِنَّ اللّهَ اشْتَرَى مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ“Hakika, Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu –wanauwa na wanauwawa.”  [At-Taubah: 111]. Rasulullah (saw) alisema: «مَنْ مَاتَ وَلَمْ يَغْزُ وَلَمْ يُحَدِّثْ بِهِ نَفْسَهُ مَاتَ عَلَى شُعْبَةٍ مِنْ نِفَاقٍ» “Yule aliyekufa lakini hakupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu wala hawakuonyesha hamu ya Jihad amekufa kifo cha mfaniki.” [Sahih Muslim]. «مَا أَحَدٌ يَدْخُلُ الْجَنَّةَ يُحِبُّ أَنْ يَرْجِعَ إِلَى الدُّنْيَا وَلَهُ مَا عَلَى الْأَرْضِ مِنْ شَيْءٍ إِلَّا الشَّهِيدُ، يَتَمَنَّى أَنْ يَرْجِعَ إِلَى الدُّنْيَا فَيُقْتَلَ عَشْرَ مَرَّاتٍ لِمَا يَرَى مِنْ الْكَرَامَةِ» “Hakuna atakayeingia Jannah atatamani kurudi katika hii dunia hata kama atapewa vyote vilivyomo duniani, isipokuwa shahidi. Kwani atatamani arudishwe duniani ili auliwe mara kumi kutokamana na hadhi atakayopewa kwa kupata shahada.” [Bukhari and Muslim].

Pili, lazima tuwalinganie waziwazi wanachuoni Waislamu ili wapaze sauti zao dhidi ya uvamizi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na wakati huohuo walinganie kupinduliwa/kutolewa mamlakani watawala vibaraka wa kikoloni ili kusimamisha tena Khilafah. Kwa kuongezea, kuwafichua wale wanaodai kuwa ni wanachuoni lakini kiuhalisia, ni wasambazaji uovu kwa kufanya kazi na maadui wa Uislamu na Waislamu. 

Tatu, lazima tuendelee kuweka sawa na kuboresha mikakati na mbinu za amali za Da’wah na kwa mpigo kufanyakazi nje na ndani ya mtandao. Cha muhimu zaidi ni kuuchochea moyo na kuulainisha. Hivyo basi, uweze kufufuka na kujikita katika suala la al-Aqsa kuwa ni la itikadi ya Kiislamu dhidi ya wanaoeneza propaganda wazalendo kuwa ni suala la Waarabu kama linavyoelekezwa na Wamagharibi wakoloni na washirika wao. Hivyo basi, Ummah wa Waislamu wazitizame Amerika, Uingereza na jamii ya kimataifa kuwa imeungana dhidi yake na kwamba ni lazima waungane chini ya Khalifah kama mlezi na mlinzi. Nabii (saw) alisema: «إِنَّ الْمُؤْمِنَ لِلْمُؤْمِنِ كَالْبُنْيَانِ، يَشُدُّ بَعْضُهُ بَعْضًا»‏‏.‏ وَشَبَّكَ أَصَابِعَه “Muumini wa kweli kwa muumini wa kweli ni kama jiwe katika ukuta, wanapeana nguvu.” Akisema (hivyo) Mtume (saw) ameshikamanisha viganja vyake na kupitisha vidole baina yake. [Bukhari 481].

Fursa kubwa na za muda mrefu ni:

Mwanzo, lazima kwa uwazi pasina kuhofia matokeao, tuwalinganie majeshi ya Waislamu kuwapindua/kuwaondosha watawala vibaraka wa kikoloni ndani ya ulimwengu wa Uislamu. Wao ndio vikwazo katika kunyanyuka kwa Uislamu na Waislamu. Kwa pamoja na mabwana zao Wamagharibi wakoloni wanapiga njama na kutekeleza sera na sharia ovu zinazokwenda kinyume na al-Qur’an Kareem na Sunnah. Hivyo basi, kusababisha madhara makubwa katika kila nyanja ya maisha.

Pili, majeshi ya Waislamu kutoa ba’yah (kiapo ch utiifu) kwa mwanamume Musilamu ili kuchukua nafasi iliyowazi baada ya kupinduliwa/kutolewa mtawala kibaraka wa kikoloni. Masharti ya ba’yah ni kutawala kwa mujibu wa al-Qur’an na Sunnah. Mwanamume Muislamu atakuwa Khalifah, ambaye serikali yake ni ile ya Khilafah iliyosimamishwa tena kwa njia ya Utume.

Tatu, haraka upesi Khalifah mpya anatangaza Jihad dhidi ya umbile la Kiyahudi na washirika wake. Hivyo basi, kufuatiwa na ukombozi wa ardhi zote za Waislamu ikijumuisha sio tu Ardhi yetu kipenzi Iliyobarikiwa ya Palestina, Kashmir na nyinginezo. Na wakati huo huo akitoa usalama kwa raia kindani kwa kutekeleza Uislamu kwa ukamilifu katika kila nyanja ya maisha. Khilafah itaitupa sharia ya kimataifa iliyo na sumu katika debe la taka.

Nne, lazima tuendelee kuwa imara na subira katika kipindi chote cha hatua hizo tatu hapo juu. Mwenyezi Mungu (swt) alisema: ﴿وَاسْتَعِينُواْ بِالصَّبْرِ وَالصَّلاَةِ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلاَّ عَلَى الْخَاشِعِينَ “Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu [kwa Mwenyezi Mungu].” [Al-Baqarah: 45].

Wakati ni sasa wa kuchukua msimamo ili kuleta Mabadiliko ya Kiislamu ya Kimataifa Yanayosubiriwa kwa sababu kila kitu sasa kiko wazi kwa kila mtu kushuhudia. Kila mmoja amechukua safu yake kwa maana wanaomuunga mkono Shetani wakiongozwa na Amerika na washirika wake na wale wanaomuunga mkono Mwenyezi Mungu (swt) na Nabii Wake (saw) wakiongozwa na Hizb ut Tahrir na wanaoiunga mkono duniani kote.

Uamuzi ni wa mtu binafsi lakini una matokeo ndani ya hii dunia ya muda mfupi na Akhira ya milele. Upande utakaochagua kuunga mkono katika kipindi hichi cha janga ni kama kujifunga kitanzi shingoni mwako. Kitanzi hicho kinaweza kuwa ni tiketi yako ya Jannah au Jahannam. ﴿مَّن يَشْفَعْ شَفَاعَةً حَسَنَةً يَكُن لَّهُ نَصِيبٌ مِّنْهَا وَمَن يَشْفَعْ شَفَاعَةً سَيِّئَةً يَكُن لَّهُ كِفْلٌ مِّنْهَا وَكَانَ اللّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ مُّقِيتًا “Mwenye kusaidia msaada mwema ana fungu lake katika hayo, na mwenye kusaidia msaada muovu naye ana sehemu yake katika hayo.  Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza na ujuzi juu ya kila kitu.” [An-Nisa: 85].

Mwishowe, washindi watakuwa ni waumini Waislamu walioko upande wa Mwenyezi Mungu (swt): ﴿وَيَقُولُونَ مَتَى هَذَا الْفَتْحُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ * قُلْ يَوْمَ الْفَتْحِ لَا يَنفَعُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِيمَانُهُمْ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ“Wanasema: Ushindi huu ni lini, kama mnasema kweli? * Sema: Siku ya Ushindi, wale walio kufuru imani yao haitawafaa kitu, wala wao hawatapewa muhula.” [As-Sajdah: 28 – 29]. Kwa kuongezea, Mwenyezi Mungu (swt) asema: ﴿وَعْدَ اللَّهِ لَا يُخْلِفُ اللَّهُ وَعْدَهُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ “Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. Lakini watu wengi hawajui.” [Ar-Rum: 6]. Bishara njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt): ﴿وَأُخْرَى تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِّنَ اللَّهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ “Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu; na wabashirieni waumini.” [As-Saf: 13].

Kwa kuhitimisha, Salahuddin ibn Yusuf ibn Ayyub baada ya kuisaifisha Bait al-Maqdis (al-Aqsa) kutokamana na Masalabiyyun, aliapa, ‘Enyi Mayahudi hamuwezi kurudi tena lau kutakuwepo na wanaume miongoni mwetu.’ Wewe ni mwanamume?!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro (Abu Taqiuddin)

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu