- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:
Kampeni ya Kitengo cha Wanawake katika Kumbukumbu ya Miaka 102 ya Kuvunjwa Khilafah
“Mabadiliko ya Kweli ni kwa kupitia Ulinganizi wa Khilafah Pekee”
"Je, Khilafah ni Ndoto Isiyowezekana?"
Ili kufuatilia Matangazo ya Moja kwa Moja
Video ya Uzinduzi wa Kampeni
Dunia iko katika machafuko. Nchi zinatumbukia katika mgogoro baada ya mgogoro chini ya tawala zilizoundwa na binadamu - ambazo zote zimethibitisha kutokuwa na uwezo wa kutatua matatizo ya binadamu. Umaskini, njaa, mauaji ya halaiki, uonevu, ufisadi, vita visivyo na maana, ukaliaji kimabavu, kusambaratika kwa familia, kuenea kwa uhalifu, unyanyasaji dhidi ya wanawake, migogoro ya afya na elimu, maisha yenye uharibifu, na matatizo mengine yanayokumba nchi kutoka mashariki hadi magharibi. Je, tutayamaliza vipi haya yote? Je, tunatokaje kwenye kinamasi hiki?
Mabadiliko ya kweli hayawezi kupatikana kwa kurudisha mzunguko wa mifumo iliyofeli - demokrasia au mengineyo. Mabadiliko haya hayawezi kufikiwa kwa kutoa tu marekebisho ya sehemu au suluhu za viraka kwa mifumo hii ya sasa yenye kasoro. Badala yake, inahitaji mabadiliko makubwa, ya msingi na ya kina.
Inahitaji kuzaliwa kwa mfumo badali unaobeba masuluhisho ya kihakika kwa matatizo ya binadamu, Inatutaka sisi kama Waislamu kuregea katika yale ambayo Mwenyezi Mungu ametuitia kwayo: Hukmu na mfumo Wake... na kuutabanni ujumbe wa Uislamu... ili kuasisi uongozi wa kweli kwa ajili ya wanadamu...
Khilafah kwa njia ya Utume
Katika mwezi wa Rajab, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kinazindua kampeni ya kimataifa yenye kichwa:
"Mabadiliko ya Kweli ni kwa kupitia Ulinganizi wa Khilafah Pekee"
Kampeni hii itaonyesha jinsi Khilafah kwa njia ya Utume itakavyozihuisha nchi za Kiislamu na kuzitoa katika hali ya machafuko na hasara zinamoishi, na kuonyeesha dhima iliyo juu yao ya kuleta mabadiliko ya kweli katika nchi zao na dunia kwa jumla. Kampeni hii pia itadhihirisha iwapo mabadiliko msingi na kusimamishwa kwa Khilafah ni ndoto tu au ni uhalisia unaoweza kufikiwa.
Tunatoa wito kila mtu anayetaka kuona mustakabali mwema kwa nchi za Kiislamu na ulimwengu huu, kuunga mkono kampeni hii muhimu, ambayo inaweza kufuatiliwa katika anwani zifuatazo:
FB – QANITATHT2
Twitter – @WSHARIAHA
Instagram – @WOMEN_SHARIA
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Jumatatu, 01 Rajab Tukufu 1444 H – 23 Januari 2023 M
- Kufuatilia Kampeni Hii kwa Lugha Nyenginezo -
Kiarabu | Kiingereza |
Kituruki | Kijerumani |
Kiurdu | Fuatilia na Usambaze |
Ushiriki wa Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina
Katika Amali za Kumbukumbu ya Miaka 102 ya Kuvunjwa Khilafah
Jumapili, 28 Rajab 1444 H - 19 Februari 2023 M
Kalima ya Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka 102 ya Kuvunjwa Dola ya Khilafah
Jumatatu, 01 Rajab Tukufu 1444 H – 23 Januari 2023 M
- Alama Ishara za Kampeni -
#ReturnTheKhilafah |
#KhilafaBringsRealChange |
#YenidenHilafet |
#HakikiDeğişimHilafetle |
#Time4Khilafah |
#TurudisheniKhilafah |
#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي |
#كيف_تقام_الخلافة |
#أقيموا_الخلافة |
Ni Nini Kitaleta Mabadiliko ya Kweli katika Ulimwengu wa Kiislamu?
Ardhi za Waislamu zimekumbwa na mlima wa migogoro na matatizo. Umaskini uliokithiri, ukosefu wa ajira kwa wingi, udikteta dhalimu, uhalifu, kuvunjika kwa familia, unyanyasaji dhidi ya wanawake, miondoko ya maisha yenye uharibifu, vijana wa Kiislamu kuwa mbali na Dini yao, na mengine mengi yanalisibu eneo hili, kwa kuakisi kile kinachoendelea katika nchi mbalimbali duniani.
Kufuatia Mapinduzi ya Kiarabu, wengi walikuwa na matumaini ya macheo mapya ya ustawi, usalama na uadilifu kuenea katika ardhi za Kiislamu.
Hata hivyo, la kusikitisha hili halikutokea.
Mjadala huu wa jopo utashughulikia jinsi mabadiliko ya kweli yanaweza kusababishwa katika ulimwengu wa Kiislamu na kile kinachohitajika ili kutatua migogoro mingi na matatizo ambayo watu wanakabiliana nayo katika eneo hili.
Ili Kusoma Taarifa ya Kitengo cha Wanawake
Ambayo Ilitangaza Kuzinduliwa kwa Kampeni Yake ya Kimataifa
Katika Kumbukumbu ya Miaka 102 ya Kuvunjwa Dola ya Khilafah
“Mabadiliko Halisi ni kwa kupitia Ulinganizi wa Khilafah PEKEE”
Jumatatu, 01 Rajab Tukufu 1444 H – 23 Januari 2023 M
Bonyeza Hapa Kufuatilia Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:
- Matoleo -
Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir Wilayah ya Tunisia Mustakabali wa Vizazi vya Vijana nchini Tunisia... Pazia la Sheria Fisadi na Mfumo wa Elimu Uliofeli Yaonyesha Mgogoro wa Kimfumo |
- Taarifa kwa Vyombo vya Habari -
|
|
Je, Lini Wanawake wa Kiislamu Watampata Mwenye Kuitikia Wito wao?! |
- Makala, Habari na Maoni -