Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ufyonzaji wa Urasilimali

Habari:

Utaratibu wa ufuatiliaji wa serikali 'wa upande mmoja', madai ya mabwenyenye wa sukari na zaidi ya yote ufichaji umesababisha ongezeko la karibu Rs20 kwa kilo kwa bei ya sukari katika siku 15 zilizopita pekee, na kuwaacha watu waliokumbwa na mfumko wa bei wakiwa hawana chaguo ila kununua bidhaa hiyo kwa viwango vya juu. (Dawn News)

Maoni:

Watu wengi bado wanatumia muda mwingi wakiwa wamekwama wakitamani siku za nyuma, wakiota mchana juu ya kipindi kifupi cha mafanikio ambacho urasilimali ulileta. Lakini zile zinazoitwa Zama za Dhahabu sasa zimeondoka muda mrefu kuliko zilivyodumu, na ulimwengu uliotokana nazo haupo tena.

Urasilimali huahidi watu maisha bora ya milele, na kila wakati huning'iniza karoti mpya mbele yao. Unaahidi kulifanya tabaka la kati kuwa matajiri na wenye kuheshimiwa na kuwa na bahati lakini urasilimali wenyewe hufanya kutowezekana kwa wengi wa tabaka la kati kufikia hili, kwa sababu lengo lake ni kuwatajirisha warasilimali, sio mtu mwengine yeyote. Matokeo yake ni aina ya pengo kati ya matarajio ya matumaini ya watu, na hali zao mbaya, kwani urasilimali hula kupitia mapato yao, akiba, kazi, majiji, miji, jamii, maadili, desturi, ili kuwatajirisha warasilimali.

Kipindi kati ya 2008 na 2020 kinaashiria zaidi ya muongo mmoja wa shida kwa uchumi wa kiulimwengu. Mnamo 2008, Mporomoko Mkubwa wa Uchumi ulishambulia, maafa ya msururu wa hasara zenye thamani ya matrilioni ya dolari na kudhoofu kwa ukuaji wa uchumi. Mnamo 2020, Covid-19 aliwasilisha pigo jengine lenye nguvu kwa mpangilio wa uchumi wa kiulimwengu. Takwimu zingine, hata hivyo, zinachora picha ya kutatanisha. Mnamo 2009, utajiri wa Jeff Bezos (mwanzilishi wa Amazon) ulikuwa $ 6.8 bilioni. Mnamo 2020, utajiri wake unasimama katika $184 bilioni! Mnamo 2009, utajiri wa Mark Zuckerberg (mwanzilishi wa Facebook) ulikuwa $2bilioni. Mnamo mwaka wa 2020, utajiri wake unasimama katika $103bilioni! Katika kipindi hicho hicho, utajiri wa matajiri 400 wa Kiamerika uliongezeka kutoka $1.27 trilioni mnamo 2009 hadi $3.2 trilioni mnamo 2020.

Benki ya Uswisi UBS iliripoti kuwa katika kilele cha Covid-19, kutoka Aprili hadi Julai 2020, matajiri zaidi ulimwenguni waliona utajiri wao ukipanda kwa asilimia 27 hadi $10.2 trilioni. Wakati huo huo, makadirio ya Benki ya Dunia yanaonyesha kuwa kwa mara ya kwanza tangu 1998, umasikini wa hali ya juu unatarajiwa kuongezeka huku watu zaidi ya milioni 115 wakianguka katika kigawanyo hicho. Kwa kuongezea, mgao wa kazi katika mapato ya kiulimwengu umekuwa ukishuka tangu angalau miaka ya 1970.

Karne ya 20 ilishuhudia kuongezeka kwa 'urasilimali wa kifedha' huku mashirika ya kifedha yakiwa kitovuni mwake. Bidhaa na biashara zao zinategemea hesabu tata na mipangilio iliyo chini ya tathmini ya mali. Suala kuu, hata hivyo, kutokana na mageuzi haya ya urasilimali ni kwamba sio wengi wanaelewa utendaji kazi wake. Huku biashara daima zimekuwa zikishikiliwa na hata maskini zaidi, urasilimali wa kifedha unaweza kuwa vigumu kuukamata hata kwa mwerevu zaidi.

Kinachotatanisha zaidi ni ukweli kwamba faida kubwa hupatikana kwa wachache tu. Kuweka mambo katika mtazamo, zingatia kwamba ilichukua kuporomoka kwa Himaya kama ya Roma ili kuanzisha athari kubwa za kiuchumi. Katika karne ya 21, ilichukua kuporomoka kwa kampuni mbili tu (Bear Stearns na Lehman Brothers) kwenye kona ya New York ili kuanzisha tukio baya ambalo halikunyoa tu mamilioni ya dolari kutoka kwa utajiri wa kiulimwengu na Pato la Taifa (GDP), lakini pia ilisababisha kuenea kwa ukosefu wa kazi.

Waumini wa kweli zaidi katika ndoto ya Urasilimali ambao wao, pia, siku moja, watakuwa Warasilimali - wameachwa wakitembea chini. Lakini pindi watu ambao wametarajia kutembea juu kwa ghafla wanaposhuka chini, kwa kawaida hawawezi kuamini, kuchakata, na kuelewa. Uhalisia wao umechanika. Sisi sote ni wahasiriwa wa Urasilimali, Urasilimali wenyewe umesababisha janga ambalo limetuacha katika kizungumkuti cha kutarajia maisha bora – badala yake kupata mabaya zaidi.

Kwa kila mtu kwa jumla, na haswa kwa Waislamu, wakati umefika sio tu wa kuuliza kufaa kwa mfumo wa kisekula na muundo wake fisidifu wa kiuchumi badala yake wafanye kazi ya kusimamisha Khilafah ambayo nidhamu yake wa kiuchumi inapeana kipaumbele mahitaji ya watu wote wanaoishi chini ya kivuli chake, tofauti na Urasilimali na kutotoa njia kwa kipote cha matajiri wachache kupata faida kubwa kupitia kuhalalisha ufisadi kupitia sheria zilizotungwa na mwanadamu. Nidhamu ya kiuchumi iliyojengwa juu ya dhahabu na fedha na isiyokuwa na riba hata chembe, ambayo haiporomoki kwa sababu ya kirusi, na ambayo hutoa ujasiri kwa watumiaji katika jamii. Uhakikishaji mzunguko wa utajiri ndio lengo la msingi la uchumi wa Kiislamu, tofauti na Urasilimali. Lengo sio kulimbikiza utajiri mwingi zaidi, wala kukua kila wakati. Mahitaji ya kimsingi ya watu lazima yatimizwe kabla ya yote mengine.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Mohammad Adel

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 13 Januari 2021 15:35

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu