Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Watoto Barani Ulaya Waanikwa kwa Maonyesho Machafu ya Televisheni

Habari:

Kampuni ya huduma ya umma inayomilikiwa na serikali ya Denmark DR, imezindua kipindi cha televisheni cha  vibonzo kwenye chaneli yake ya watoto "DR Ramasjang", kinacho onyesha mwanaserere wa uongo kama mwanamume mwenye sehemu kubwa ya siri, ambayo inaonekana katika kila kipindi. Kikundi kinacholengwa kinatangazwa kuwa watoto kutoka umri wa miaka 4 hadi 8. Mkurugenzi wa ubunifu wa silsila  hizo za vibonzo anadai kuwa mpango huo unatakiwa "kuangazia udadisi wa watoto wa ujinsia na mwili wa mwanadamu". Chaneli hiyo hiyo ilifanya onyesho jengine hivi karibuni, ambapo watoto walikuwa walianikwa kutazama watu wazima walio uchi, ikidaiwa kuwa kama mbinu ya elimu kuhusu mwili wa mwanadamu. Nchi nyingine za Ulaya kama vile Uholanzi zimesifu onyesho hilo.

Maoni:

Jamii za Magharibi mara nyingi husifiwa kama zilizoathiriwa pakubwa na ngono. Denmark inajulikana haswa kwa ukombozi wa ngono uliofanyika kuanzia miaka ya 60 na 70, ambapo ponografia ya watoto ilihalalishwa. Denmark pia ilikuwa nchi ya kwanza kuhalalisha ponografia, na mitaala ya kielimu na vyombo vya habari zinaathiri pakubwa watoto kwa kile kinachosifiwa kama mtazamo wa Kideni juu ya uvumilivu na uhuru.

Katika nchi za Ulaya kama Uingereza na Denmark, watoto hupitia elimu ya ngono mapema kuanzia shule ya msingi. Haya ni majaribio ya kuwavua watoto haya na aibu ambayo ni sehemu asili ya maumbile yao (fitra). Wanasaikolojia hutetea vipindi kama hivyo, katuni, na vichekesho kama vya kujifurahisha na mbinu za kujifunza, ambazo huwachochea watoto moja kwa moja kuchunguza ujinsia na kwa sababu hiyo kufahamu matusi na uchafu, huku ikidhaniwa ni kuwafundisha watoto kujua jema na baya.

Jamii za Magharibi haziwezi kutofautisha jema na baya, wala kitamaduni, kimaadili, au kupitia sheria, na matatizo mengi ya utamaduni huria hupuuzwa kwa jina la uhuru wa kibinafsi. Je! Mtu anawezaje kutarajia kipindi cha Runinga kilichoundwa kwa matusi kuwafundisha watoto mema na mabaya?

Wanasiasa wa Kimagharibi kwa kweli walikuwa chini ya uangalizi katika vyombo vya habari, kwa sababu ya visa kadhaa vya unyanyasaji wa kijinsia wa wanasiasa wa kiume kwa wanawake, kwa kuongeza mjadala unaoendelea juu ya vuguvugu la #MeToo. Kesi hizi zilifichuliwa na wanawake wengi, ambao ima walishinikizwa kutotajwa, au kufichua wazwazi kesi zao, wengine hata baada ya kimya cha miaka mingi. Kwa kipindi cha wiki moja, wanasiasa wawili mashuhuri walikuwa wameacha nyadhifa zao, baada ya kufichuliwa kwa umma na vyombo vya habari. Kesi hizi zinaelezea hadithi mbaya ya mtazamp mbaya juu ya wanawake, ambayo umenasibishwa na tabia huria inayotokana na thaqafa ya Kimagharibi na uhuru wa kibinafsi.

Katika Uislamu, Haya, kujistiri na zinaa na kulinda maisha ya familia ni mambo msingi katika kulea watoto, ambayo kwayo vizazi vijavyo hulindwa. Pia inawalinda watoto kutokana na mada zisizowahusu, ili uzuri wao usiharibiwe. Thaqafa ya Kimagharibi inaonyesha upotovu wake mara kwa mara, na ni dhahiri kuwa hakuna wema au thamani inayopatikana katika thaqafa hii, ambayo inawalazimishwa Waislamu kwa njia mbali mbali.

Uislamu ni ujumbe mtukufu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt), ambao Waislamu wanashikamana nao imara. Uislamu una suluhisho kwa matatizo yote ya wanadamu, ikiwemo misiba ya kijamii, kiakili, na kimaadili ambayo imeenea Magharibi, ikiwemo Denmark.

]فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا فِطْرَتَ اللَّهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّهِ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini – ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo nyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui. [Al-Rum:30]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Younes Piskorczyk

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 13 Januari 2021 15:59

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu