Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 18/06/2022

China Yazindua Chombo cha Kubeba Ndege cha Kwanza cha Nyumbani

Kwa mujibu wa gazeti la ‘The Washington Post’:

China ilizindua chombo chake cha kwanza cha kubeba ndege kilichoundwa nyumbani mnamo siku ya Ijumaa, chombo chenye teknolojia ya hali ya juu ya kurusha ndege sawa na wenzao wa Marekani, katika hafla iliyowekwa kuashiria kupanuka kwa uwezo wa kijeshi wa nchi hiyo ...

Vyombo viwili vya kwanza vya uchukuzi vya China ikiwemo uregeshaji wa modeli ya zamani ya Kisovieti, Liaoning, iliyonunuliwa kutoka Ukraine mnamo 1998, na Shandong, ambayo iliundwa nchini China lakini kwa msingi wa modeli ya Liaoning na kuanza kutumika mnamo 2019.

Fujian inawakilisha hatua kubwa mbele katika teknolojia na uwezo, wachambuzi wanasema.

Ingawa chombo cha kubeba ndege hakitafanya kazi kikamilifu kwa angalau miaka kadhaa, tayari kinazua tumbojoto. Ridzwan Rahmat, mchambuzi katika kampuni ya upelelezi ya Janes, aliiambia AP:

"Hii inaonyesha kwamba wahandisi wa Kichina sasa wanaweza kutengeneza kundi kamili la vyombo vya kivita vinavyohusishwa na vita vya kisasa vya majini, ikiwa ni pamoja na corvettes, frigates, destroyers, meli za mashambulizi aina ya amphibious, na sasa chombo cha kubeba ndege.

Uwezo huu wa kuunda meli madhubuti ya kivita kuanzia chini kabisa bila shaka utasababisha mabadiliko na manufaa mbalimbali kwa tasnia ya ujenzi wa meli ya China.

Ukuaji wa China unabeba mafunzo muhimu kwa wale wanaofahamu miongoni mwa Umma wa Kiislamu. Ukuaji wa uchumi wa China haukuwa pambano kamwe kwa Magharibi, mradi uchumi wa China umejengwa kwa mtindo wa mauzo ya nje unaohudumia mahitaji ya watumiaji wa Magharibi. Kampuni nyingi za Amerika zilihamisha utengenezaji wao hadi China. Nchi za Magharibi ziliinyonya China kwa nguvu kazi nafuu ya kiwandani kama ilivyoendelea kunyonya makoloni yake ya zamani kote ulimwenguni. Nguvu za kiuchumi haziwezi kujengwa kwa mtindo unaolenga kusafirisha nje, kuhudumia mahitaji ya wengine huku tukipuuza mahitaji yetu wenyewe. Ukuaji wa China sasa unakuwa tishio kwa Magharibi kwa sababu wameanza kujenga uchumi wao kwa matakwa ya nyumbani, ya kijeshi.

Nchi za Waislamu leo ​​zimesalia katika mfumo wa uchumi wa kikoloni ingawa imepita miongo kadhaa tangu ukoloni rasmi kumalizika. Badala ya Magharibi kuchimba bidhaa, rasilimali na vibarua kwa nguvu, tunasafirisha nje bidhaa hizi zote kwao kwa hiari tukifikiri kwamba haya yote yanatunufaisha.

Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Ummah wa Kiislamu hivi karibuni utainuka na kupindua urithi wa utawala wa kikoloni katika ardhi zetu, na kusimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Mtume (saw), ambayo itaziunganisha tena ardhi za Waislamu, na kuyakomboa maeneo yake yaliyokaliwa kwa mabavu, kutabikisha Sharia ya Kiislamu, kuregesha mfumo wa maisha wa Kiislamu na kubeba nuru ya Uislamu kwa ulimwengu mzima. Dola ya Khilafah, tangu kuanzishwa kwake, itajiunga na safu za dola kuu kutokana na ukubwa wake, idadi kubwa ya watu, rasilimali nyingi, jiografia isiyo na kifani na mfumo wa kipekee wa Kiislamu. Dola ya Khilafah itajenga kikamilifu uchumi wake juu ya mahitaji ya ndani, hususan mahitaji ya kijeshi, hivyo kuharakisha kunyanyuka kwake kama dola kuu.

Biden Yu Chini ya Shinikizo juu ya Ziara ya Saudia

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters:

Rais wa Marekani Joe Biden alisema mnamo siku ya Ijumaa kuwa hatasafiri kwenda Saudi Arabia kwa uwazi kukutana na kiongozi halisi Mohammed bin Salman wakati wa safari mwezi ujao na akasema anamwona mfalme mtarajiwa wa Saudia kama sehemu ya "mkutano mpana wa kimataifa".

Mipango ya Biden ya kumuona mfalme huyo mtarajiwa, anayejulikana kama MBS, ni sehemu ya safari yake ya kwanza katika eneo la Ghuba kama rais. Amekosolewa na wabunge wa Marekani, wakiwemo baadhi ya chama chake cha Democrat na watetezi wa haki za binadamu, ambao wanasema kuwa ziara hiyo inakinzana na ahadi yake ya kuweka haki za binadamu katika moyo wa sera ya kigeni ya Marekani.

"Sitakutana na MBS. Naenda kwenye mkutano wa kimataifa, na atakuwa sehemu yake," Biden aliwaambia waandishi wa habari mnamo Ijumaa alipoulizwa ni vipi katika safari yake ya Saudi Arabia atashughulikia mada ya 2018 ya mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Jamal Khashoggi, mkazi wa Marekani na mkosoaji wa mfalme huyo mtarajiwa.

Rais anasafiri kuelekea Saudi Arabia kwa mwaliko wa Mfalme Salman pamoja na wakuu wengine wanane wa nchi kwa ajili ya Mkutano wa GCC+3, msemaji wa Baraza la Usalama wa Kitaifa alisema.

Biden alianza muhula wake wa urais kwa kujitenga na sera za mtangulizi wake wa chama cha Republican, Donald Trump. Ilikuwa kwa msingi huu ambapo Wamarekani walipiga kura kwa wingi kumchagua Biden badala ya kuchaguliwa tena kwa Trump. Lakini bila shaka, demokrasia ya ‘uwakilishi’ ya Magharibi kwa kweli ni demokrasia iliyosimamiwa tu; haijalishi ni mtu gani amechaguliwa, wote wanafuata kimsingi njia sawa ya kuendeleza maslahi ya Marekani; demokrasia ‘halisi’, haipo popote pale, wazo la demokrasia, ambapo watu wanajitawala wenyewe, ni la kindoto sawa na kusema kwamba watoto wa shule wanapaswa kujielimisha wenyewe, au kwamba askari wanapaswa kujiamuru wenyewe, au kwamba wafanyakazi wa kampuni wanapaswa kujisimamia wenyewe.

Marais wa Marekani hujaribu tu kujitenga hadharani kutoka kwa viongozi kama vile Mohammad bin Salman kwa sababu ya mwitikio wa kisiasa wa ndani ya Amerika. Lakini ukweli ni kwamba viongozi kama vile mawakala wa Marekani kikamilifu, hutekeleza tu ajenda ya Marekani. Biden alijua wazi kwamba ingemlazimu, wakati fulani, kuzuru Saudi Arabia na kukutana na watawala wake. Kwa miezi kadhaa, amekuwa akijaribu kutumia kupanda kwa bei ya mafuta kama kisingizio cha kufanya hivyo. Sasa ana kisingizio cha ziada cha kushiriki katika ‘mkutano wa kimataifa’.

Biden ndiye rais wa Marekani mwenye uzoefu zaidi katika miongo mitatu. Ambapo marais wengi huacha mipango mikuu ya sera za kigeni hadi nusu ya pili ya muhula wao, Biden ametimiza kiasi kikubwa sana ndani ya miezi 18 yake ya kwanza: kujiondoa kutoka Afghanistan, kuihusisha Urusi nchini Ukraine, na kuelekeza nguvu zaidi kwa China. Lakini kwa sababu malengo ya sera ya kigeni ya Amerika lazima yafichwe kutoka kwa umma wake, watu wa Amerika hawajui mafanikio ya Biden, na anaonekana kuwa na uungwaji mkono mdogo sana.

Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Dola ya Khilafah hivi karibuni itasimamishwa na malengo yake ya sera za kigeni yatawiana kikamilifu na matarajio ya Ummah kwa mujibu wa Sharia ya Kiislamu, na kumwezesha Khalifa kutenda kwa kujiamini na nguvu kamili. Mtume (saw) amesema katika Hadith tukufu iliyopokelewa na Abu Hurayrah (ra): «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»“Imam ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujihami kwayo.”[Sahih Muslim: 1841].

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu