Kwa Kutangaza Maombolezi ya Kitaifa Juu ya Kifo cha Malkia Elizabeth II, Serikali ya Hasina Ilifichua Utiifu wake Halisi kwa Waingereza na Kusaliti Damu na Muhanga wa Watu Waliopigania Ukombozi kutoka kwa Ukoloni wa Kiingereza
- Imepeperushwa katika Bangladesh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Serikali ya Hasina ilitangaza Maombolezi ya kitaifa ya siku tatu kutokana na kifo cha Malkia wa Uingereza Elizabeth II. Bendera ya taifa itawekwa nusu mlingoti katika mashirika yote yanayomilikiwa kikamilifi na serikali, yenye kumilikiwa nusu na serikali na mashirika huru, taasisi za elimu, majengo yasiyo ya serikali, na balozi za Bangladesh ng’ambo, kulingana na arifa iliyotolewa na Kitengo cha Baraza la Mawaziri.