Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 515
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan itaanzisha tena kikao cha kila mwezi, Jukwaa la Masuala ya Ummah, ambalo linajadili masuala ya Ummah na kuwasilisha masuluhisho ya kimsingi kwa kuzingatia imani ya Ummah, itikadi tukufu ya Kiislamu.
Sherehe zilienea katika miji mingi nchini Sudan jana, Jumamosi, 28/9/2024, mjini Shendi, Atbara, Port Sudan, na kwengineko. Sherehe hizo hata zilivuka mipaka ya Sudan hadi Misri kwa furaha kwa ushindi wa jeshi na kuingia kwake katika kiwanda cha kusafisha mafuta cha Al Jaili kaskazini mwa Khartoum, ingawa habari hiyo haijathibitishwa hadi taarifa hii kwa vyombo vya habari ilipoandikwa.
Miezi michache iliyopita, wafungwa 23 wa zamani wa kisiasa walihukumiwa huko Tashkent. Ilibainika kuwa 15 kati yao waliainishwa kama “wahalifu hatari sana wa kurudia” na walihukumiwa vifungo vya miaka 7 hadi 14, kutumikia katika kituo maalum cha kizuizi cha serikali. Wanane waliosalia walihukumiwa kifungo cha nyumbani kwa hadi miaka 5.
Enyi askari katika ardhi za Waislamu: Je, hakuna miongoni mwenu mwenye hekima? Ambaye anawaongoza askari, hasa kutoka katika nchi ya Misri (Kinanah), Ash-Sham na ardhi ya Al-Fatih, ili majeshi yaliyosalia yamfuate, yakiimba Allahu Akbar, ili Ummah ufuate Takbira hizo nyuma yao kwa ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt)?
Nchini Uswidi, babu na bibi sasa wanapokea pesa kutoka kwa serikali kwa ajili ya kuwatunza wajukuu zao. Sheria inayohusiana na hili ilianza kutumika msimu huu wa joto.
Ushiriki wa Muislamu katika Demokrasia ni jambo lenye kuwashughulisha watawala, wanasiasa, wasomi na watungaji sera. Hii ni ima Waislamu wakiwa katika Ulimwengu wa Kiislamu, au wakiishi ughaibuni katika nchi za Magharibi. Hivyo kuna mjadala kuhusu ushiriki wa Muislamu katika Demokrasia nchini Australia, Uingereza na Amerika, kama ulivyo mjadala kuhusu ushiriki wa Waislamu katika uchaguzi nchini Uturuki, Pakistan na Misri.
Bangladesh na mfumo wa sasa wa ulimwengu… Darubini ya Kiislamu!
Kwa kuzingatia mapambano yanayoendelea, ni wazi kuwa masuluhisho ya sasa yanayoongozwa na Amerika yanashindwa kushughulikia sababu kuu za mzozo huo. Hafla hii itavinjari mwelekeo tofauti-uliojikita katika kanuni na uadilifu wa Kiislamu-ili kutoa njia ya mabadiliko ya kudumu.
Katika wiki za hivi karibuni, Global Ikhwan Sdn Bhd (GISB) imekabiliwa na uchunguzi mkali kutoka kwa mamlaka kufuatia wasiwasi wa muda mrefu juu ya desturi zake potovu. Ingawa ripoti zilikuwa zimewasilishwa dhidi ya GISB mapema zaidi, hatua za hivi majuzi za polisi zinaashiria hatua ya kwanza muhimu ya kupunguza shughuli za kundi hili. GISB, ambayo mizizi yake inatoka kwenye vuguvugu la Al-Arqam ambalo sasa limezimika, imevutia umakini wa watu wengi kwa kulingania vitendo vya upotofu vya Aurad Muhammadiyah na madai ya utovu wa nidhamu, hasa katika uendeshaji wa nyumba za misaada.