Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 516
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir / Uholanzi iliandaa matembezi katika mji mkuu wa Uholanzi, Amsterdam, kwa mnasaba wa kupita mwaka mmoja kamili wa vita vya mauaji ya Halaiki dhidi ya Waislamu wa mji wa Gaza Hashem, kunusuru na kuiombea nusra na Izza Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na Gaza.
Wabunge nchini Kenya wameanza mchakato wa kumwondoa naibu rais wa nchi hii afisini. Wale wanaounga mkono juhudi hizo wanamshutumu Rigathi Gachagua kwa kuhusika katika maandamano ya Juni ya kupinga serikali - ambayo yaligeuka kuwa mabaya - pamoja na kuhusika katika ufisadi, kuhujumu serikali na kuendeleza siasa za mgawanyiko wa kikabila. Naibu rais amepuuzilia mbali madai hayo.
Rais wa Marekani Joe Biden alikutana na kiongozi wa mpito wa Bangladesh Muhammad Yunus pembezoni mwa mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa, katika kuonyesha uungaji mkono baada ya maasi kuiangusha serikali ya kiimla ya Hasina.
Msimamo dhaifu wa watawala wa Pakistan ni kwa sababu ya ubaraka wao kwa Amerika. Hata kabla ya kuisalimisha Kashmir kwa India mnamo Agosti 2019, watawala wa Pakistan hawakuwa makini kuhusu ukombozi wa Kashmir Inayokaliwa kimabavu. Watawala wa Pakistan walifuata tu sera ya Amerika ya kutoa shinikizo kwa India, ili iingie kwenye kambi ya Amerika. Baada ya India kuingia katika kambi ya Marekani kupitia kundi tawala la Hindutva, watawala wa Pakistan waliachana na Kashmir Inayokaliwa kimabavu ili kuifurahisha Amerika.
Imepita mwaka mmoja tangu jeshi la watu waoga zaidi katika uso wa dunia kuanza mauaji ya halaiki huko Gaza. Mnawezaje bado kukubali kudhalilishwa, vifo na uharibifu kama huu uliowekwa juu ya watu wenu, mbele ya macho yenu? Vipi bado mnaweza kubaki tuli, ilhali ni kwa kupitia nguvu za mikono yenu ndipo Ummah unatafuta ulinzi wake? Je, mwanajeshi anaweza kukubali ukuu wa kijeshi wa adui yake, bila kufyatua risasi hata moja? Je, askari anawezaje kukataa kupigana na adui yake, na kudumisha Dini yake, heshima na uanaume wake imara?
Sera ya Marekani kwa Ulimwengu wa Kiislamu ni sera ya kuwatiisha na kuwadhalilisha Waislamu, kwa kuungwa mkono na kuwatia nguvu maadui wa Ummah. Kuhusu Pakistan haswa, Marekani inataka kuidhoofisha Pakistan ili kuruhusu India kuinuka, ili Dola hiyo ya Kibaniani iweze kukabiliana na Waislamu na China kwa niaba yake.
Licha ya kupita siku nyingi, watawala wa Pakistan bado hawajajibu ipasavyo hatua hatari ya India kuhusiana na Mkataba wa Maji wa Indus (IWT), makubaliano ya kugawanya maji yaliyosimamiwa na Benki ya Dunia mnamo 1960. Mnamo 18 Septemba 2024, India ilituma notisi rasmi kwa Pakistan, ikitaja masuala mbalimbali, ikiwemo mabadiliko ya idadi ya watu, changamoto za kimazingira, na mambo mengine, ikiomba kutathminiwa upya kwa mkataba huo. India imeripotiwa kutuma barua nne tangu Januari 2023, ikitaka uhakiki.
Tangu kuzuka mapinduzi ya Umma nchini Tunisia mwishoni mwa mwaka 2010, Hizb ut Tahrir imesisitiza kuwa mradi pekee wa kihadhara wenye uwezo wa kuyafanikisha mapinduzi hayo na kufikia matakwa ya wanamapinduzi unatokana na kuupindua utawala wa kisekula na badala yake kuubadilisha kwa mfumo adilifu wa kisiasa, na hili linaweza tu kufanywa kupitia Uislamu, chini ya dola moja; dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Mnamo Jumatano, Agosti 28, 2024, Jenerali Michael Langley, Kamanda wa Kamandi ya Amerika ya Afrika (AFRICOM), alisema wakati wa mkutano wake na Waziri wa Ulinzi wa Tunisia Khaled El-Suhaili kwamba Tunisia iko mstari wa mbele katika nchi za Kiafrika zenye ushirikiano wa kihistoria na wa kipekee. Marekani, ikielezea utayari wake wa kuendeleza na kupanua mahusiano haya. Ziara hii inajiri siku tatu baada ya kuapishwa kwa wajumbe wa serikali.