Kwa Kuregea kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Tutamaliza Vita, Sio kupitia Mazungumzo Yanayofadhiliwa na Marekani, Adui wa Uislamu na Waislamu!
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Baada ya wiki tatu za mauaji na uharibifu, Marekani inaamuru watu wake wafanye mazungumzo jijini Jeddah baada ya mamia kuuawa, maelfu kujeruhiwa, miundombinu kuharibiwa, maisha kuvurugika, watu kuhamishwa kutoka kwa makazi yao, kutangatanga, kuzingirwa na kifo, njaa na magonjwa.