Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu Waislamu wa Uyghur
- Imepeperushwa katika Uholanzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Afisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imetoa ripoti kuhusu uzito wa "ukiukwaji wa haki za binadamu" dhidi ya Waislamu wa Uyghur unaofanywa na China. Afisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu (OHCHR) inasema kuwa imepata ushahidi wa kutosha wa mateso na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu ambao unaweza kuelezewa kama "jinai dhidi ya binadamu".