Jumatatu, 27 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kongamano la Cairo Larudisha tena Utawala ule ule Uliosababisha Migogoro na Kuichana Nchi

Jana, Jumamosi, tarehe 6 Julai 2024, lile linaloitwa Kongamano la Kisiasa na Majeshi ya Kiraia ya Sudan lilifanyika katika mji mkuu wa Misri, Cairo; nukta muhimu katika taarifa ya mwisho zilizotolewa zilikuwa: “...wanakongamano pia walisisitiza ulazima wa kushikamana na Azimio la Jeddah na kuzingatia taratibu za utekelezaji na maendeleo yake ili kuendana na maendeleo katika vita…

Soma zaidi...

Uchaguzi nchini Marekani na Uingereza Unashindana katika Kulenga Uislamu na Waislamu

Katikati ya uungaji mkono wa Marekani na Uingereza kwa mauaji yanayofanywa na umbile la Kiyahudi, ambalo liliasisiwa na Himaya ya Uingereza yenyewe, na baada ya zaidi ya miezi tisa ya uungaji mkono wao kwa umwagaji damu wa Waislamu mjini Gaza, kampeni za uchaguzi wa rais na chama zinaendelea hivi sasa nchini Marekani na Uingereza.

Soma zaidi...

Utiifu Wakuendelea kwa India unathibitisha kwamba Serikali ya Hasina ni Tishio kwa Ubwana wa Nchi; na Wajibu wa Vikosi vya Jeshi, Mlinzi wa Ubwana huu, ni kuiondoa mara moja Serikali ya Hasina

Ili kuonyesha uaminifu wake usioyumbayumba kwa India, Hasina aliondoka bila kuchelewa hadi New Delhi (Juni 21, 2024) kukutana na Waziri Mkuu mpya aliyechaguliwa wa India. Katika ziara hii, Hasina alitia saini Mikataba 10 ya Maelewano (MoU) kwa ajili ya India.

Soma zaidi...

Masuluhisho Yaliyopendekezwa kwa Gaza ya baada ya Vita

Huku vita vya mauaji ya halaiki vya umbile la Kiyahudi, kwa uungaji mkono muovu wa Marekani ya Magharibi, vikiendelea dhidi ya watu wa Gaza kwa zaidi ya miezi mitano, na wahanga wake kufikia zaidi ya mashahidi na majeruhi 100,000, pamoja na kuangamizwa kwa sehemu kubwa ya majengo yake, kuna mazungumzo mengi kuhusu miradi ya massuluhisho ya kile kitakachokuja baada ya vita vya Gaza na jinsi mambo yatakavyokuwa kisiasa kulingana na mipango ya dola za kikoloni zikiongozwa na Marekani.

Soma zaidi...

Kwa Nini Wafungwa wa Kisiasa wa Zamani Wanakamatwa Tena?

Vijana 23 wanaoshtakiwa kwa sasa huko Tashkent wote wamekuwa gerezani kwa zaidi ya miaka ishirini na hawajaregea kwa familia zao kwa muda mrefu. Ni wanaume mashujaa wa zama zetu waliotaka kufuata Dini yetu kikamilifu, hawakukaa kimya mbele ya ukandamizaji, na kisha wakatuhumiwa kwa sababu ya fikra na imani zao, wakistahamili karibu robo karne ya mateso yasiyo ya kibinadamu kizuizini.

Soma zaidi...

Barua kwa Raisi wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev

Tunamwambia Bw. Shavkat Mirziyoyev: Mashababu wote wa Hizb ut Tahrir wanaozuiliwa katika magereza ya Uzbekistan, ambao kwa sasa wako katika kesi, wanaofanyiwa uchunguzi, au wanaoishi uhamishoni, ni Wauzbekistani. Mwenyezi Mungu amewapa haki kamili ya kutoa maoni yao kwa manufaa ya nchi hii... Zaidi ya hayo, ulipochukua urais, ulikula kiapo kwenye muundo huo wa kikatiba uliothibitisha haki ya kujieleza na kuabudu. Hivyo basi, utawala haujashikamana na amri ya Mwenyezi Mungu wala muundo huo wa kikatiba kiutendaji!

Soma zaidi...

Wakenya Amkeni

Kenya, shamba la kikoloni, kwa mara nyingine imo katika mchafuko na mtikisiko kwa kuwa mchezo wa bahati nasibu wa kidemokrasia umezunguka nyuzi 360! Walioko madarakani na walioko barabarani wakiandamana wanalaumiana, huku madai yakielekezwa kwa Mswada wa  Kifedha wa 2024 ulioandaliwa kwa maelekezo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) (Business Daily, 28 Juni 2024)! Mswada huo unapendekeza mikakati ya kuzidisha ukusanyaji wa ushuru ambao unatajwa kuwa ni wenye kukandamiza na kuwadidimiza  raia katika umasikini zaidi!

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu