Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 508
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Matembezi ya 44 mfululizo yalifanyika tangu kuanza kwa Vita vya Kimbunga cha Al-Aqsa, yakianzia mbele ya Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu wa Tunis, hadi barabara ya Al-Thawra, ambayo yaliitishwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kwa watu wa Al-Zaytouna, na kichwa chake kilikuwa “Majeshi ya Afrika Kaskazini lazima yajiandae dori yao katika kuikomboa Palestina”.
Kisimamo cha Usiku “Kuna tofauti gani kati ya mshirika na mwongo mdanganyifu?!”
Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.
IMF ni taasisi ya kikoloni, na dori yake ni kudumisha utawala wa dolari ya Marekani kote duniani kupitia sera zake za kiliberali za uchumi mamboleo.
Watu wa Bangladesh—zaidi ya 92% yao ni Waislamu na sehemu ya mojawapo ya Waislamu wengi zaidi duniani—wamejitokeza katika maandamano ya amani yanayoongozwa na wanafunzi dhidi ya dhalimu Sheikh Hasina. Maandamano ya hivi punde yalizuka baada ya serikali inayoongozwa na Hasina kujaribu kuongeza mgawo wa nafasi za kazi serikalini kwa kuwapendelea wafuasi watiifu wa serikali badala ya wagombea wenye sifa stahiki. Sera hii ni ya hivi punde tu katika mfululizo wa vitendo vya rushwa na uonevu vinavyofanywa na serikali ya Awami League tangu iingie mamlakani mwaka wa 2009.
Baada ya juhudi zilizoratibiwa za Wazayuni zenye lengo la kukashifu sauti zinazoiunga mkono Palestina, zilizoundwa na mfululizo wa makala ya magazeti ya udaku na vipindi vya TV vinavyofafanuliwa kwa batili na dosari, ilidhihirika kwamba wengi wao hawakustahili jibu la heshima hata kidogo.
Baada ya majuma kadhaa ya ukandamizaji wa kikatili dhidi ya watu wa Bangladesh na dhalimu Hasina, genge la serikali yake, na wachungaji wake wa kigeni, alilazimishwa kidhalilifu kuikimbia nchi. Waislamu shupavu wa Bangladesh, wakiongozwa na wanafunzi jasiri, walivumilia ukatili usio na kifani na hatimaye kulazimisha kuondolewa kwake kupitia wimbi lisilozuilika la maandamano ambayo yalimshinda dikteta huyo.
Kwa nini Waziri Mkuu hataki kuwa muwazi kwa wananchi kuhusu jinsi watu watalazimika kumudu kifurushi hiki kipya.