Jarida la UQAB Toleo 85 - Februari 2024
- Imepeperushwa katika Jarida la UQAB
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir Wilayah ya Kenya imechapisha toleo jipya la Jarida la UQAB kwa ajili ya mwezi wa Februari 2024 M.
Hizb ut Tahrir Wilayah ya Kenya imechapisha toleo jipya la Jarida la UQAB kwa ajili ya mwezi wa Februari 2024 M.
Ujumbe wa matarajio na ukakamavu katika kujibu tuhma za uongo zilizofanywa dhidi ya Hizb ut Tahrir.
Mnamo tarehe 25 Januari 2024, gazeti la Sudan Tribune liliripoti kuhusu Mpango wa Mahitaji na Muitikio wa Kibinadamu wa 2024 kwa ajili ya kusimamia idadi kubwa zaidi ya watu waliokimbia makaazi yao. Kwa sasa, Wasudan milioni 14.7 wamelazimika kuyahama makaazi yao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka mwaka wa 2023.
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) mnamo Jumanne ilishutumu ujenzi na uzinduzi wa 'Ram Mandir' iliyojengwa kwenye eneo la Msikiti wa Babri Masjid wenye umri wa karne tano huko Ayodhya nchini India.
Mnamo Jumatano, Januari 17, 2024, shirika la Bloomberg la Marekani lilifichua kushindwa kwa Washington kufikia mkakati wake unaolenga kuifunga Bahari Nyekundu kwa urambazaji. Shirika hilo lilitaja kuwa takriban meli 114 na meli za mafuta zilivuka Bab el Mandeb mnamo Jumatano iliyopita, siku tano baada ya uvamizi wa majini uliofanywa na vikosi vya kijeshi vya Marekani na Uingereza katika Bahari Nyekundu.
Jana Januari 23, 2024, kupitia tukio la kufutwa kazi mwalimu mmoja wa Chuo Kikuu cha BRAC kwa kupinga kuingizwa kwa watu waliobadili jinsia (jinsia ya 3 iliyotajwa kwenye kitabu) “Hadithi ya Sharifa” katika darasa la saba kitabu cha “Historia na Sayansi ya Kijamii” cha mtaala mpya, kwa mara nyengine tena msururu wa njama za kuharibu imani na maadili ya kizazi chetu kijacho cha Umma wa Kiislamu umejitokeza.
Msemaji wa Afisi ya Rais wa Jamhuri, Ahmed Fahmy, alithibitisha kuwa dola hii imepata mafanikio mengi katika ngazi na nyanja zote na kueleza kuwa serikali inajitahidi kukabiliana na changamoto hizo akisema: “Ni jambo la kimaumbile kwa wananchi kuhisi afueni inayotokea wakati utabikishaji umekamilika na juhudi zote kuwekwa wazi.”
Rais Erdogan, katika taarifa yake baada ya kikao cha baraza la mawaziri, alisema: “Mashaka juu ya utawala wa Uturuki ni mjadala uliomalizika kwa kuishangilia Jamhuri mnamo Oktoba 29, 1923. Hakuna mtu yeyote katika nchi hii ambaye ana tatizo na jamhuri au mwanzilishi wa taifa.”
Waziri wa Fedha Jibril Ibrahim, kwa mara ya tano mfululizo, aliongeza kwa ujasiri bei ya dolari ya forodha, ambayo ilianza kuongezeka mnamo Juni 2021, kutoka pauni 28 hadi pauni 370, kisha hadi pauni 445, kisha hadi pauni 564, kisha hadi pauni 650.
Kisimamo kwa Anwani “Mapinduzi Hayatainama, Ewe Fidan, hata kama Yatasalitiwa na Wasaliti Elfu Moja”