Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Ikiwa Sera ya Mambo ya Nje ni Kufanya Urafiki na Adui, Basi Ziara ya Adui Hakika Itakaribishwa!

Inasikitisha kwamba Malaysia inaendelea kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na China (na pia Urusi), licha ya ukatili uliothibitishwa na ukandamizaji unaofanywa na nchi hiyo ya kikomunisti dhidi ya Waislamu wa Uighur kwa miongo kadhaa. Mbali na uhusiano wa kidiplomasia, Malaysia pia imeanzisha uhusiano mkubwa wa kibiashara na China, na kuifanya kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa nchi hiyo.

Soma zaidi...

Kuhusu Kesi ya Mahakama ya Rufaa ya Wafungwa wa Zamani wa Kisiasa

Kama tulivyotaja awali, mahakama ya rufaa inaendesha kesi ya wafungwa 15 wa zamani wa kisiasa huko Tashkent. Wanaume kumi na watano kati ya 23 (Mashababu), ambao awali walifungwa miaka 20 kwa fikra na imani zao, walihukumiwa mnamo Julai mwaka huu kifungo cha kuanzia miaka 7 hadi 14, wengi wao walihukumiwa kifungo katika kituo maalum cha uzuizi cha serikali.

Soma zaidi...

Uislamu Pekee ndio Utakaonusuru Wanadamu na Ukandamizaji wa Kodi

Mfumo wa uchumi wa kibepari hutegemea kodi kandamizi pekee kama chanzo kikuu cha mapato. Katika hali hiyo inatarajiwa serikali daima itabuni na kulazimisha kodi mbalimbali ambazo ni wazi zitakuwa mzigo kwa raia wa kawaida. Serikali za kidemokrasia za kibepari badala ya kufanya bidii kuondoa mzigo wa kodi, zenyewe zihakikisha kila mtu analipa kodi.

Soma zaidi...

Enyi Wanajeshi wa Kiislamu, Je, Hakuna Salahuddin Mpya Miongoni Mwenu? Kukuongozeni Katika Kuwanusuru Mashahidi na Kuliondoa Umbile la Kiyahudi?

Je, hakuna miongoni mwenu Abdul-Hamid, mlinzi wa Palestina kutokana na Mayahudi… ambaye alimrudisha mwakilishi wao akiwa amekata tamaa na kushindwa, bila kupata chochote, na akamfundisha somo la hekima, akisema: “Siwezi kupeana hata shubiri moja ya ardhi ya Palestina?, kwani sio mali yangu, bali ni mali ya Ummah wa Kiislamu. Watu wangu waliipigania ardhi hii na kuinywesha kwa damu yao… Mayahudi nawabakie na mamilioni yao, kwani ikiwa Dola ya Khilafah itasambaratika siku moja, basi hapo wanaweza kuichukua Palestina bila thamani yoyote, lakini maadamu niko hai, hilo halitafanyika…”?

Soma zaidi...

Heshima ya Wanawake wa Kiislamu ni ya Khiyari katika Demokrasia za Kiliberali

Mnamo tarehe 3 Oktoba, CBS News iliripoti kwamba mwanamke mmoja Muislamu alizuiliwa na polisi wa Philadelphia ambao walimvua hijabu yake. Wakati wa saa 20 ya kukamatwa kwake, aliachwa wazi na hakupewa njia ya kubadilisha nguo zake. Kwa sasa ameajiri mshauri wa kisheria kutoka Baraza la Mahusiano ya Kiislamu la Marekani (CAIR) na anataka haki kwa unyanyasaji wake.

Soma zaidi...

Mauaji Mapya na Msimamo wa Majeshi yetu ni Ule Ule! Je, hakuna Mwenye Hekima Miongoni mwenu Awezaye Kurudisha Izza Tena?!

Mwenyezi Mungu Mtukufu alitufahamisha kuwa sisi ni Umma wa kheri na jihad, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitupa bishara njema ya kwamba tutaifungua Roma, kwa hivyo Al-Quds iko karibu na ukombozi, Mwenyezi Mungu akipenda, kuwa mji mkuu wa dola inayokuja ya Khilafah, na historia kwa mapana yake yote inathibitisha kwamba sisi ni Ummah ambao hata tukilala kwa muda gani, tutaamka na kuwaondoa maadui zetu kwa pigo kubwa ambalo baada ya hapo hawana pa kukimbilia.

Soma zaidi...

Biden Asherehekea Kuuwawa kwa Yahya Al-Sinwar!

Katika taarifa yake ya kina, Rais Joe Biden alithibitisha kwamba ujasusi wa Marekani ulisaidia “Israel” kumpata na kumlenga Yahya Al-Sinwar, pamoja na viongozi wengine wa Hamas waliojificha chini ya ardhi. “Kwa marafiki zangu wa Israel, hii ni siku ya afueni na tafakari, sawa na mandhari nchini Marekani baada ya Rais Obama kuamuru uvamizi wa Osama Bin Laden mwaka wa 2011,” Biden alisema. “Yahya Al-Sinwar alikuwa kizuizi kikubwa cha amani. Kizuizi hicho sasa kimeondoka, lakini kazi nyingi inabaki mbele.”

Soma zaidi...

Operesheni ya Kishujaa ya Wanajihadi Hossam na Amer Dhidi ya Wanajeshi wa Kiyahudi Inakanusha Udhuru Wowote kwa Jeshi Kushindwa Kuchukua Hatua dhidi ya Umbile lao

Vitendo hivi vya kishujaa vya kibinafsi, kukabiliana na adui muoga kwa kuvuka mipaka, na kuuawa kishahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu ili kuyakomboa maeneo matakatifu, Msikiti wa Al-Aqsa, na Palestina yote kutoka kwa Mayahudi na Amerika, ambayo inaendelea kuwapa silaha, vifaa, na ujasusi huku likieneza ufisadi, vinapaswa kuchochea ndani yenu hisia ya heshima na uanaume. Nyinyi watu wenye nguvu mnaoitwa “ndugu wenye silaha” mnapaswa muinuke kumtetea Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na Waislamu, na sio watawala wenu wanaowapeleka kwenye maangamivu na kuwatumikisha kwa maadui zenu.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu