Ijumaa, 27 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Nani Anayeishajiisha Kyrgyzstan Kuondoka kutoka katika Ushawishi wa Putin?

Mnamo Oktoba 9, IA 24.KG, ikitoa mfano wa Wizara ya Ulinzi ya Kyrgyzstan, iliripoti kwamba mazoezi ya "Udugu Usioweza Kuvunjika - 2022" huko Balykchy yalifutiliwa mbali. "Amri na mazoezi ya majeshi "Udugu Usioweza Kuvunjika - 2022", ambayo yalipaswa kufanywa kuanzia Oktoba 10 hadi 14 katika kituo cha mafunzo cha Edelweiss cha kitengo cha kijeshi Na. 20636 huko Balykchy, yalifutiliwa mbali na Wizara ya Ulinzi ya Kyrgyzstan.

Soma zaidi...

Waziri wa Fedha Hawezi Kurekebisha Uchumi wa Pakistan Unaodhibitiwa na IMF

Waziri wa Fedha wa Pakistan, Bw. Ishaq Dar mnamo Jumapili, tarehe 16 Oktoba 2022, aliusihi Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na wafadhili wa kimataifa kutoa usaidizi mkubwa wa kisera. Aliiomba IMF kuunda muitiko wake kuafikiana na hali ya Pakistan na nchi zilizo na hali kama hiyo kwa kuzingatia changamoto kubwa za kiuchumi, kijamii na kisiasa zinazokabiliana nazo huku kukiwa na majanga yanayosababishwa na tabianchi, kulingana na taarifa moja kwa vyombo vya habari iliyotolewa na wizara ya fedha.

Soma zaidi...

Tukio la Kifedha la Uingereza

“Mnamo Ijumaa asubuhi, Chansela wa Hazina ya Uingereza, Kwasi Kwarteng, aliitwa siku moja kabla kurudi London kutoka Marekani moja kwa moja hadi Downing Street, ambako aliachishwa kazi yake. Hatua hiyo ilikuja wiki tatu baada ya Kwarteng kutangaza bajeti ndogo yenye utata iliyojaa hatua za kupunguza ushuru ambazo hazijafadhiliwa zilizopelekea masoko ya fedha kudorora.

Soma zaidi...

Porojo za Vita Dhidi ya Ugaidi Zinaendelea

Mnamo Jumatatu tarehe 19/09/2022 Tanzania iliungana na nchi nyingine za Afrika katika kutekeleza Itifaki ya Mkataba wa Umoja wa Afrika (AU) wa Kuzuia na Kupambana na Ugaidi. Baada ya kupitishwa azimio la kuridhiwa kwa itifaki hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yusuph Masauni alisema kuwa Tanzania ina nafasi kubwa ya kupata manufaa kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao na kurahisisha ubadilishanaji wa taarifa za kiintelijensia kuhusu ugaidi kupitia ushirikiano wa karibu kutoka kwa nchi wanachama.

Soma zaidi...

Uoanishaji wa Waislamu nchini Denmark Unahusiana na Maadili na Imani, Sio Kazi wala Elimu

Mnamo tarehe 30 Septemba, Wizara ya Uhamiaji na Uoanishaji ya Denmark ilichapisha ripoti ya hali ya kile kinachojulikana kama kipimo cha uoanishaji. Kipimo hicho cha uoanishaji kilichapishwa mnamo 2012, na kinakusudiwa kuonyesha maendeleo katika uoanishaji wa wahamiaji wasio wa Kimagharibi ndani ya malengo kama vile kazi, elimu na lugha.

Soma zaidi...

Wanawake na Watoto wa Kiislamu Wanakumbwa na Njaa Hadi Kufa Nchini Somalia huku Watawala wa Waislamu Wakiunga Mkono Ukandamizaji Ulimwenguni

Mnamo tarehe 5 Oktoba 2022, BBC iliripoti kuwa Somalia inakabiliwa na baa la njaa inayotokana na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40. Hadithi ya dada mmoja Muislamu inayofichuliwa na waandishi wa habari, ni ile ya Fatima Omar ambaye alimzika mtoto mmoja wa kiume kutokana na njaa na tayari alikuwa ameshamzika bintiye wa miaka 3 ambaye alifariki huku akitembea kwa siku 10 kutafuta msaada. Anawaambia waandishi wa habari kwamba hakuwa na nguvu za kumzika mtoto wake na alilazimika kuuacha mwili wake kando ya barabara huku akijua kuwa Fisi walikuwa wanakaribia kuingia ndani.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu