Vijana wa Kashmir wanapotea katika Giza la Uraibu wa Madawa ya Kulevya bila Nuru ya Khilafah
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 5 Juni, BBC iliripoti juu ya "ongezeko la kutisha la matumizi mabaya ya dawa za kulevya huko Kashmir". Wajana wa kiume zaidi na zaidi wanaweza kupatikana nje ya kituo pekee cha kutibu uraibu katika eneo la Kashmir linalosimamiwa na India, wakiwa kwenye foleni na wazazi wao kupokea dawa kutoka kwa Taasisi ya Afya ya Akili na Sayansi ya Nyuroni (IMHANS) ili kusaidia kupunguza dalili zao za kujiondoa katika uraibu na kuzuia maambukizi ya magonjwa ya kuambukiza.